uhura / sw_gen_train.json
ebayes's picture
Upload 30 files
597042a verified
[
{
"q": "Kuna mililita ngapi kwenye lita 1?",
"a": "1000",
"context": "",
"grade": "4",
"category": "Mathematics"
},
{
"q": "Tunajuaje kwamba Vanessa hakukata tamaa? Taja sababu mbili.",
"a": "[\"Kusimama nje ya ofisi za serikali peke yake\", \"Aliwasaka wabunge (na kuwataka wabadili sera)/alihusisha serikali\"]",
"context": "",
"grade": "GCSE",
"category": "Reading comprehension"
},
{
"q": "Utajumlisha nambari gani na 526 ili jawabu iwe 666?",
"a": "140",
"context": "",
"grade": "4",
"category": "Mathematics"
},
{
"q": "Kuna ushahidi gani kwamba vijana wanapenda kuwa sehemu tofauti wakati mmoja. Taja mbili.",
"a": "1. Hauwezi kupita muda wa saa moja bila kuingia kwenye mitandao tofauti ya kijamii\n2. Huwa na akaunti tano au zaidi kwenye majukwaa tofauti.",
"context": "Wiki iliyopita shule yetu ilitembelewa na Bwana Musa. Yeye ni Mkenya na anafanya utafiti katika chuo kikuu huko Nairobi. Mada ya utafiti wake ni ‘matumizi ya mitandao ya kijamii kwa vijana’. \n\nAlipofika tu, alianza kwa kutuuliza maswali yaliyokuwa na lengo la kuchunguza mienendo na matumizi yetu ya mitandao ya kijamii. Alitaka kujua wanafunzi wangapi huangalia simu zao za mkononi pale wanapoamka tu. Ikabainika kwamba asilimia kubwa kati yetu hufanya hivyo. Wengi wetu hufuatilia picha zinazobandikwa na husoma maoni ya watu tofauti kuhusu picha hizo. Bwana Musa akaongezea kusema kwamba ana uhakika wengi wetu huendelea kuangalia simu zetu za mkononi kila baada ya dakika chache. Hapo tena wanafunzi wengi walicheka huku wakikubaliana na maneno yake. Tena zaidi ya hapo, rafiki yangu Hadija aliongeza ‘ninapoamka tu hukuta nimeshatumiwa ujumbe kama kumi hivi kunitaka nitoe maoni kuhusu picha zilizobandikwa usiku uliopita!’ Hapo tulicheka tena tukikubaliana naye. \n\nBwana Musa alituuliza maswali mengi. Swali ambalo lilinifanya nitafakari kuhusu mambo yanayonivutia linahusu chakula. Aliuliza, ‘wanafunzi wangapi hupiga picha za vyakula kabla ya kuvila?’ Ilibidi ninyooshe kidole na kusema mimi hufanya hivyo. Nilimfahamisha kwamba, pale ninapotembelea mikahawa na kula vyakula vilivyopambwa vizuri, mimi hupendelea kuvipiga picha. Pia hufanya hivyo ninapoviona vyakula ambavyo hupikwa kwa nadra. Siku hizi hata mama yangu haturuhusu kula kabla ya yeye mwenyewe kupiga picha huku akitania ‘hakuna ruhusa ya kula kabla ya kuvipiga picha vyakula’. \n\nBwana Musa alitufahamisha kwamba, maisha tuliyoyazoea sasa ni tofauti kabisa na yale ya watu waliozaliwa miaka kumi au kumi na tano tu iliyopita. Vijana wa sasa hawathamini mazungumzo ya ana kwa ana na hawaandikiani barua kama zamani. Vijana wa sasa wanategemea mitandao ya kijamii ili kuwasiliana na wenzao. Hapo nikaelewa sababu za wazazi wangu kuniambia nipunguze matumizi ya simu. \n\nMimi nimepangiliwa muda maalumu wa kutumia simu ninapokuwa nyumbani. Muda huu ni saa kumi na moja jioni hadi saa kumi na mbili na nusu. Ninamshukuru mama yangu kwa kuupata muda huo ingawa ni mfupi. Baba yangu hapendi kabisa intaneti. Yeye husema ‘ningependelea kama intaneti isingekuwapo kabisa kwani unapotumia intaneti kwa muda mrefu unapoteza ujuzi wako wa kuzungumza kwenye jamii. Pia unajifunza upuuzi na huwi makini darasani kabisa’. \n\nKwa kiasi kikubwa, Bwana Musa alikubaliana na baba yangu kwamba intaneti ni kipingamizi darasani. Lakini alitutahadharisha kwa kusema ‘kuna umuhimu wa kutumia intaneti na mitandao ya kijamii kwani watu hupata ufahamu mkubwa wa mada tofauti na hujenga mahusiano mazuri ya kimataifa’. \n\nAlitupa takwimu chache ambazo zilinishangaza. Kwanza alisema kwamba miaka miwili iliyopita, vijana walitumia takribani saa moja kila siku kwenye mitandao ya kijamii. Pia walikuwa na akaunti moja au mbili tu. Kwa hivyo walitumia muda huo kuangalia mitandao tofauti. Hivi sasa asilimia kubwa ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii ni vijana. Alituuliza, ‘wangapi kati yenu mna uwezo wa kutotazama simu kwa zaidi ya saa zima?’ Hakuna hata mmoja wetu aliyenyoosha kidole. Halafu alituuliza, ‘wangapi kati yenu mna akaunti tano au zaidi kwenye majukwaa tofauti?’ Hapo karibu sote tulinyoosha vidole. Basi Bwana Musa alicheka na kusema, ‘mnaona, nyinyi vijana mnapenda kuwa sehemu tofauti wakati mmoja!’ \n\nMimi ninapotumia intaneti hupenda kusoma hadithi tofauti kwenye tovuti za mitandaoni. Hizi huandikwa na waandishi ambao bado hawajajulikana na huwa nzuri sana. Pia huangalia filamu au vichekesho. \n\nIngawa ninapenda kupiga picha, kwa kawaida hupendelea kubandika picha za vyakula na si picha zinazoonyesha mahala nilipo na familia yangu kwani sitaki kujihatarisha. Bwana Musa alituonya na kusema kwamba, kuna hatia nyingi za kihaini zinazofanyika kwenye mitandao. Alitufahamisha kwamba, kwenye mitandao ya kijamii, vijana hukubali maombi ya urafiki kutoka kwa watu wasiowajua. Mimi sijawahi kufanya hivyo. Alisema kwamba mara nyingi vijana hutazama picha za watu wanaowaomba urafiki na kama zinavutia basi wao hukubali ombi la urafiki. Pia wakati mwingine hutazama kama wana marafiki wa pamoja na hao watu na kukubali urafiki. Kwa hakika uamuzi huu si mzuri kwani, kiukweli, wao hawawajui watu hawa na wanaweza kuwa waovu. Mambo haya huweza kuleta madhara mengi. Mfano ni hatari ya kuibiwa na pia kupoteza usalama kutokana na vitisho tofauti. Bwana Musa alimalizia kwa kututahadharisha wote kwa kusema kwamba ni muhimu kuwa na nidhamu na pia kuwa makini.",
"grade": "GCSE",
"category": "Reading comprehension"
},
{
"q": "Toa 0.02 kwenye 0.78.",
"a": "0.76",
"context": "",
"grade": "4",
"category": "Mathematics"
},
{
"q": "Jumla ya wanafunzi 7,500 walifanya mtihani katika kituo chao. Wanafunzi 6,845 walifaulu mtihani huo. Jee, wanafunzi wangapi hawajafaulu mtihani huo?",
"a": "655",
"context": "",
"grade": "4",
"category": "Mathematics"
},
{
"q": "Matumizi makuu ya ndege zisizo na rubani:",
"a": "[\"Kutafuta vyanzo vya maji chini ya ardhi\", \"Kuchunguza afya ya mazao\", \"Kuchunguza afya ya wanyama pori na miti.\", \"Kutuma dawa.\", \"Kuchunguza ujangili\", \"Kuchunguza hali ya barabara mashambani.\", \"Kusanya data nyeti\"]",
"context": "Soma makala yafuatayo kuhusu ndege zisizo na rubani.\n\t\t\t\t\t\nHuonekana kama vidude vya kuchezea na ni marufuku katika mbuga kadhaa za wanyama kwa sababu ya sauti yake ya kukera ifananayo na nyuki. Hata hivyo, ndege zisizo na rubani zimeanza kuwa jambo la kawaida katika maisha ya kila siku. Hurushwa kutoka mbali kwa kutumia kifaa ardhini kinachoshikwa na mtu. Pia huweza kufika sehemu zisizofikika kirahisi. Kwa hivyo, ni chombo muhimu kwa mashirika mengi, ingawa huleta changamoto.\n\t\t\t\t\t\nNdege zisizo na rubani zinaweza kutumiwa kutafuta vyanzo vya maji chini ya ardhi na kuchunguza afya ya mazao. Ili kufanya hivyo, zinahitaji kupaa zikiwa karibu na ardhi huku zikipiga picha. Hata hivyo, mara nyingi huruka juu ya watu ambao hawajashauriwa na inawezekana hawajakubaliana na uwepo wao. Jambo hili linaweza kuwa na athari mbaya kwa jamii zile zile ambazo ndege zisizo na rubani zinataka kusaidia.\n\t\t\t\t\t\nMtu mmoja anayefanyia uchunguzi jambo hili ni Profesa Muturi Njeri. Anasema ‘uonekano wa ndege hizi unaweza kuleta tuhuma na wasiwasi kama watu hawajashauriwa tangu hapo awali. Watu wanazihusisha na jeshi hivyo huogopa namna ambavyo mamlaka husika yanavyoweza kuzitumia’.\n\t\t\t\t\t\nNjeri anatoa mfano wa kuhifadhi misitu, ambapo ndege zisizo na rubani zinaweza kuchunguza afya ya wanyama pori na miti. Utafiti wake unaonyesha kwamba wenyeji hawataki kuingia porini wanapofahamu uwepo wa ndege hizo. Hii ni kwa sababu wao hupata hofu, hata kama wakiwa hawafanyi jambo baya. Pia kumekuwa na ripoti za ndege hizi kuharibiwa na kudunguliwa.\n\t\t\t\t\t\nMatumizi salama\n\t\t\t\t\t\nHata hivyo, matumizi ya ndege zisizo na rubani yanazidi kukua jinsi zinavyoendelea kuwa madhubuti na kuwa na kazi tofauti. Kwa mfano, hivi karibuni Shirika la Kimataifa la Elimu na Watoto limeanza kutuma dawa nchini Malawi kwa kuzitimia. Serikali ya Afrika Kusini inazitumia kusaka majangili misituni, wakati nchi nyingi zinafuatilia hali ya barabara mashambani kwa kutumia picha zake.\n\t\t\t\t\t\nKhalid Kumbuka ni mkuu wa shirika lililopo Afrika Mashariki linalowapa wateja wao, kama wakulima na wafanya biashara, picha za viwanja vyao kutoka hewani. Amejionea mwenyewe athari chanya za ndege zisizo na rubani. Mwaka 2015, aliongoza timu yake katika mradi wa kuwaonyesha wakulima waliokuwa majirani ukubwa na mipangilio ya mashamba yao.\n\t\t\t\t\t\n‘Wakulima waliopokea picha hizo waliweza kutambua maeneo yenye nafasi za ziada ili kulima zaidi. Kwa hivyo, uzalishaji uliongezeka,’ alieleza bwana Kumbuka. ‘Zaidi ya hapo, wakulima wengi walifurahia picha hizo na kuzitundika ukutani ndani ya nyumba zao.’\n\t\t\t\t\t\nAnasema kwamba timu yake hushauriana na jamii tofauti kabla ya kutumia ndege zisizo na rubani, hata kama tayari wana kibali cha serikali. ‘Kufuatana na hayo, hatujawahi kuona kesi ambapo watu wameleta mashitaka. Kwa kawaida watu hufurahi. Wanazielewa faida na kwamba ndege inayopiga picha hufanya hivyo kwa salama.’\n\t\t\t\t\t\nMatumizi salama hayahusu kushauriana na jamii tu. Pia yanahusu data gani zinakusanywa na jinsi zinavyotumika, hasa tukizingatia kwamba ndege zisizo na rubani zina uwezo wa kupiga picha nzuri sana za watu na kukusanya data nyeti.\n\t\t\t\t\t\nKanuni za maadili\n\t\t\t\t\t\nSerikali zinafahamu hatari zinazoweza kujitokeza. Mwaka huu, nchi 42 zilikubali kuendeleza viwango vya kimataifa vya kutunza na kulinda data. Hata hivyo, sheria zinaweza kutekelezwa vibaya ndani ya nchi na hubadilika kati ya nchi tofauti. Hivi karibuni, Kenya imepiga marufuku ndege zisizo na rubani, ingawa nchi nyingine zinaziruhusu kwa ada za juu. Licha ya hayo, Njeri bado ana matumaini, kwa sababu uwepo wa sheria tofauti ni bora kuliko kutokuwa na sheria zozote.\n\t\t\t\t\t\nNjeri anataka wanaofanya utafiti wawajibike zaidi, kwa mfano kwa kutunza na kulinda data vizuri zaidi. ‘Nini kitatokea kama mtafiti akipiga picha ya shughuli haramu, au kama unapata video ya mtu anawinda tembo? Je, utaenda kushitaki polisi au utaifuta? Matatizo haya yanatakiwa yashughulikiwe mapema kwa kutumia kanuni na sera wazi.’\n\t\t\t\t\t\nKwa bwana Kumbuka, mpangilio ni muhimu kwa sifa nzuri ya kampuni yake. Mifano ya sera zao ni pamoja na kukataa kutoa picha zinazowatambulisha watu na shughuli zao. Anaamini kwamba mashirika mengi zaidi yanafuata mfano wao, ingawa bado kuna safari ndefu.",
"grade": "GCSE",
"category": "Reading comprehension"
},
{
"q": "Nauli ya daladala kwa kila abiria mmoja ni shilingi 400. Jee, kwa abiria 9 zitapatikana shilingi ngapi?",
"a": "3,600",
"context": "",
"grade": "4",
"category": "Mathematics"
},
{
"q": "Usafiri wa gari unawavutia watu gani?",
"a": "(Wenye) familia kubwa",
"context": "Kuna aina nyingi za usafiri wa kila siku. Mtu anaweza kuendesha gari, kupanda basi au treni, kukodi teksi au kutembea kwa miguu. Inaonekana kwamba siku hizi watu wengi wanapenda sana kutembea au kupanda baisikeli. Zamani watu walipopanda baisikeli au kutembea walionekana kama fukara na hawana uwezo wa kununua gari au kulipia usafiri wa umma. Siku hizi watu wanaelewa kuwa magari yanaleta uchafuzi wa mazingira, na pia kuna sababu za kiuchumi kwani kutembea na kutumia baisikeli ni bure kabisa. Hata hivyo huku kwetu bado gari linaendelea kuwa muhimu kwani watu wengine huwa na familia kubwa inayojumuisha ndugu na jamaa tofauti, kwa hivyo ni lazima kuwa na usafiri madhubuti.\n \nNilifanya utafiti pamoja na kaka yangu na tuligundua kwamba katika mji wetu, zaidi ya asilimia 50 ya watu hutumia baisikeli kama njia yao kuu ya usafiri. Kati ya hawa, wapo ambao hufanyia kazi zao kwenye baisikeli. Mfano mzuri ni wale wanaouza madafu, mboga na matunda ambayo huyapakia kwenye baisikeli zao. Wao huwa na matenga makubwa yaliyojaa bidhaa na huzunguka mitaani huku wakiuza. Zaidi ya hapo, takriban asilimia 20 ya watu hutumia baisikeli mara moja moja ili kuenda kazini au shuleni. Pia kuna asilimia ndogo ya watu ambao hupanda baisikeli kwa ajili ya mashindano.\n \nMimi ni katika watu walioshindana katika mbio za baisikeli zilizotoka Tanzania hadi Afrika ya Kusini. Sikuwa na nguo zinazotakiwa kwa ajili ya mashindano, kwani sikuwa na uwezo wa kununua mpya kwa sababu muhimu zaidi ilikuwa ni kupata baisikeli haraka. Ilibidi baba aninunulie baisikeli mpya ya mashindano. Ilikuwa ghali sana na alisema hataninunulia baisikeli nyingine kwa miaka kumi ijayo.\n \nTulipofika Afrika ya Kusini nilishangaa kuona barabara maalumu za baisikeli. Niliporudi kwetu nilimhadithia mama yangu aliyewaambia ndugu zetu ‘Salha alipokuwa kule sikuwa na wasiwasi wowote wa ajali za barabarani na sasa mimi nitakwenda naye mwaka ujao’. Mimi nitafurahi kuwa na mama yangu katika mashindano lakini ninahisi nitalazimika kuendesha polepole ili nisimwache nyuma. Yeye ameshanunua taa mpya ambazo amezibandika nyuma na mbele ya baisikeli yake. Pia amenunua mnyororo madhubuti wa kuifungia baisikeli yake ili isiibiwe.\n \nNingefurahia zaidi kama kaka yangu angekubali kuja kwani ni yeye aliyenifundisha kuendesha. Aliwaambia rafiki zake, ‘kamwe sikutegemea kwamba Salha angeenda hadi Afrika ya Kusini kwa baisikeli, safari ndefu na hatari’!",
"grade": "GCSE",
"category": "Reading comprehension"
},
{
"q": "Mwezi gani katika mwaka una siku chache?",
"a": "Februari",
"context": "",
"grade": "4",
"category": "Mathematics"
},
{
"q": "Ikiwa daftari moja lina karatasi 48. Jee, madaftari 30 yatakua na karatasi ngapi?",
"a": "1440",
"context": "",
"grade": "4",
"category": "Mathematics"
},
{
"q": "Vanessa Nakate aliahidi kujenga nini?",
"a": "Majiko [mbadala]",
"context": "Mara ya kwanza kumsikia Vanessa Nakate ilikuwa mwaka uliopita. Alitembelea shule moja kijijini kwetu na kutuambia kwamba angerudi baada ya muda mfupi na kutujengea majiko makubwa yatakayotumia nishati mbadala kupika chakula. Majiko hayo yangetumia miale ya jua. Alitueleza kwamba yeye alishasaidia shule chache kutokana na ufadhili ambao huupata sehemu tofauti. Baada ya muda mfupi, Vanessa alirudi na akajenga hayo majiko.\n\t\t\t\t\t\nAlitufahamisha kwamba, yale majiko ya kuni na mkaa tuliyokuwa tukiyatumia pale awali yalikuwa ni chanzo kikuu cha uchafuzi wa mazingira. Mimi binafsi nilishasoma shuleni kwamba ukataji wa miti ili kupata kuni za kupikia, hasa ule ukataji usiodhibitiwa, ni tishio kubwa kwa uwepo wa misitu. Na kama tujuavyo misitu ni muhimu sana kuendeleza mifumo ya maisha yetu sisi binadamu, maisha ya wanyama na pia mimea. Hivyo nilielewa kwamba alilofanya Vanessa Nakate lilikuwa jambo la muhimu sana.\n\t\t\t\t\t\nVanessa alisema kwamba ni lazima vijana wa Kiafrika washiriki katika majadiliano ya kimataifa yanayohusu mazingira. Ili binadamu waweze kuishi maisha bora, ninadhani kuna umuhimu kwetu kuhifadhi mazingira. Mara nyingi baada ya makongamano na mazungumzo ya kimataifa, vijana husikilizwa. Mashirika tofauti huamini uongozi wa vijana duniani ni suluhisho na huwapa pesa kwa miradi. Kwa njia hii, Vanessa aliweza kuanzisha kazi yake na kupambana na changamoto za mazingira.\n\t\t\t\t\t\nVanessa Nakate alizaliwa Uganda na alihitimu chuo kikuu cha Makerere akiwa na shahada ya masomo ya Biashara. Alianza kuwa mwanaharakati wa mazingira mwaka 2019 baada ya kuona vijana duniani wakijulikana kwa kuandamana huku wakikumbusha serikali zao kuchukua hatua zitakazoleta mabadiliko ya kimazingira duniani. Vanessa alifanya hivyo pia. Alianza kwa kuwaomba ndugu zake waende naye sehemu tofauti katika jiji la Kampala huku wakiwa wamebeba mabango. Mabango waliyobeba yalikuwa na maneno kama ‘mazingira ni uhai’, ‘gomea hali ya hewa’ na ‘ukipanda mti, unapanda msitu’.\n\t\t\t\t\t\nWapita njia na madereva waliwashangaa. Yeye alihisi kwamba ameweza kuongeza sauti yake kwenye mazungumzo yanayohusu mazingira. Ndugu zake waliporudi shuleni yeye aliendelea kusimama nje ya ofisi tofauti za serikali peke yake huku akipigania kusikilizwa. Aliwasaka wabunge na kuwataka wabadili sera za uwekezaji. Vanessa alitaka serikali ikabiliane na viwango vya maji katika Ziwa Viktoria ambavyo vimekuwa vikipanda na kuleta hatari ya mafuriko.\n\t\t\t\t\t\nMwishoni mwa mwaka 2019 Vanessa alianza kutambulika na kualikwa kwenye vyombo vya habari na mikutano tofauti duniani. Anasema kwamba, ‘sehemu kubwa ya dunia haina furaha kwa sababu ya mgogoro wa hali ya hewa, ninataka kuona watu wenye furaha na dunia yenye furaha’. ",
"grade": "GCSE",
"category": "Reading comprehension"
},
{
"q": "Nauli ya daladala kwa kila abiria mmoja ni shilingi 400. Jee, kwa abiria 9 zitapatikana shilingi ngapi?",
"a": "3,600",
"context": "",
"grade": "4",
"category": "Mathematics"
},
{
"q": "Uwanja wa mpira wa mnazi mmoja una urefu wa mita 800 na upana wa mita 200.Tafuta eneo la uwanja.",
"a": "160,000",
"context": "",
"grade": "4",
"category": "Mathematics"
},
{
"q": "Mama ana hisia gani kuhusu kupiga picha chakula?",
"a": "Anapenda kupiga picha",
"context": "Wiki iliyopita shule yetu ilitembelewa na Bwana Musa. Yeye ni Mkenya na anafanya utafiti katika chuo kikuu huko Nairobi. Mada ya utafiti wake ni ‘matumizi ya mitandao ya kijamii kwa vijana’. \n\nAlipofika tu, alianza kwa kutuuliza maswali yaliyokuwa na lengo la kuchunguza mienendo na matumizi yetu ya mitandao ya kijamii. Alitaka kujua wanafunzi wangapi huangalia simu zao za mkononi pale wanapoamka tu. Ikabainika kwamba asilimia kubwa kati yetu hufanya hivyo. Wengi wetu hufuatilia picha zinazobandikwa na husoma maoni ya watu tofauti kuhusu picha hizo. Bwana Musa akaongezea kusema kwamba ana uhakika wengi wetu huendelea kuangalia simu zetu za mkononi kila baada ya dakika chache. Hapo tena wanafunzi wengi walicheka huku wakikubaliana na maneno yake. Tena zaidi ya hapo, rafiki yangu Hadija aliongeza ‘ninapoamka tu hukuta nimeshatumiwa ujumbe kama kumi hivi kunitaka nitoe maoni kuhusu picha zilizobandikwa usiku uliopita!’ Hapo tulicheka tena tukikubaliana naye. \n\nBwana Musa alituuliza maswali mengi. Swali ambalo lilinifanya nitafakari kuhusu mambo yanayonivutia linahusu chakula. Aliuliza, ‘wanafunzi wangapi hupiga picha za vyakula kabla ya kuvila?’ Ilibidi ninyooshe kidole na kusema mimi hufanya hivyo. Nilimfahamisha kwamba, pale ninapotembelea mikahawa na kula vyakula vilivyopambwa vizuri, mimi hupendelea kuvipiga picha. Pia hufanya hivyo ninapoviona vyakula ambavyo hupikwa kwa nadra. Siku hizi hata mama yangu haturuhusu kula kabla ya yeye mwenyewe kupiga picha huku akitania ‘hakuna ruhusa ya kula kabla ya kuvipiga picha vyakula’. \n\nBwana Musa alitufahamisha kwamba, maisha tuliyoyazoea sasa ni tofauti kabisa na yale ya watu waliozaliwa miaka kumi au kumi na tano tu iliyopita. Vijana wa sasa hawathamini mazungumzo ya ana kwa ana na hawaandikiani barua kama zamani. Vijana wa sasa wanategemea mitandao ya kijamii ili kuwasiliana na wenzao. Hapo nikaelewa sababu za wazazi wangu kuniambia nipunguze matumizi ya simu. \n\nMimi nimepangiliwa muda maalumu wa kutumia simu ninapokuwa nyumbani. Muda huu ni saa kumi na moja jioni hadi saa kumi na mbili na nusu. Ninamshukuru mama yangu kwa kuupata muda huo ingawa ni mfupi. Baba yangu hapendi kabisa intaneti. Yeye husema ‘ningependelea kama intaneti isingekuwapo kabisa kwani unapotumia intaneti kwa muda mrefu unapoteza ujuzi wako wa kuzungumza kwenye jamii. Pia unajifunza upuuzi na huwi makini darasani kabisa’. \n\nKwa kiasi kikubwa, Bwana Musa alikubaliana na baba yangu kwamba intaneti ni kipingamizi darasani. Lakini alitutahadharisha kwa kusema ‘kuna umuhimu wa kutumia intaneti na mitandao ya kijamii kwani watu hupata ufahamu mkubwa wa mada tofauti na hujenga mahusiano mazuri ya kimataifa’. \n\nAlitupa takwimu chache ambazo zilinishangaza. Kwanza alisema kwamba miaka miwili iliyopita, vijana walitumia takribani saa moja kila siku kwenye mitandao ya kijamii. Pia walikuwa na akaunti moja au mbili tu. Kwa hivyo walitumia muda huo kuangalia mitandao tofauti. Hivi sasa asilimia kubwa ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii ni vijana. Alituuliza, ‘wangapi kati yenu mna uwezo wa kutotazama simu kwa zaidi ya saa zima?’ Hakuna hata mmoja wetu aliyenyoosha kidole. Halafu alituuliza, ‘wangapi kati yenu mna akaunti tano au zaidi kwenye majukwaa tofauti?’ Hapo karibu sote tulinyoosha vidole. Basi Bwana Musa alicheka na kusema, ‘mnaona, nyinyi vijana mnapenda kuwa sehemu tofauti wakati mmoja!’ \n\nMimi ninapotumia intaneti hupenda kusoma hadithi tofauti kwenye tovuti za mitandaoni. Hizi huandikwa na waandishi ambao bado hawajajulikana na huwa nzuri sana. Pia huangalia filamu au vichekesho. \n\nIngawa ninapenda kupiga picha, kwa kawaida hupendelea kubandika picha za vyakula na si picha zinazoonyesha mahala nilipo na familia yangu kwani sitaki kujihatarisha. Bwana Musa alituonya na kusema kwamba, kuna hatia nyingi za kihaini zinazofanyika kwenye mitandao. Alitufahamisha kwamba, kwenye mitandao ya kijamii, vijana hukubali maombi ya urafiki kutoka kwa watu wasiowajua. Mimi sijawahi kufanya hivyo. Alisema kwamba mara nyingi vijana hutazama picha za watu wanaowaomba urafiki na kama zinavutia basi wao hukubali ombi la urafiki. Pia wakati mwingine hutazama kama wana marafiki wa pamoja na hao watu na kukubali urafiki. Kwa hakika uamuzi huu si mzuri kwani, kiukweli, wao hawawajui watu hawa na wanaweza kuwa waovu. Mambo haya huweza kuleta madhara mengi. Mfano ni hatari ya kuibiwa na pia kupoteza usalama kutokana na vitisho tofauti. Bwana Musa alimalizia kwa kututahadharisha wote kwa kusema kwamba ni muhimu kuwa na nidhamu na pia kuwa makini.",
"grade": "GCSE",
"category": "Reading comprehension"
},
{
"q": "Salha alipaswa kufanya nini ili kushiriki katika mashindano?",
"a": "Kununua/Kununuliwa baisikeli (haraka)",
"context": "Kuna aina nyingi za usafiri wa kila siku. Mtu anaweza kuendesha gari, kupanda basi au treni, kukodi teksi au kutembea kwa miguu. Inaonekana kwamba siku hizi watu wengi wanapenda sana kutembea au kupanda baisikeli. Zamani watu walipopanda baisikeli au kutembea walionekana kama fukara na hawana uwezo wa kununua gari au kulipia usafiri wa umma. Siku hizi watu wanaelewa kuwa magari yanaleta uchafuzi wa mazingira, na pia kuna sababu za kiuchumi kwani kutembea na kutumia baisikeli ni bure kabisa. Hata hivyo huku kwetu bado gari linaendelea kuwa muhimu kwani watu wengine huwa na familia kubwa inayojumuisha ndugu na jamaa tofauti, kwa hivyo ni lazima kuwa na usafiri madhubuti.\n \nNilifanya utafiti pamoja na kaka yangu na tuligundua kwamba katika mji wetu, zaidi ya asilimia 50 ya watu hutumia baisikeli kama njia yao kuu ya usafiri. Kati ya hawa, wapo ambao hufanyia kazi zao kwenye baisikeli. Mfano mzuri ni wale wanaouza madafu, mboga na matunda ambayo huyapakia kwenye baisikeli zao. Wao huwa na matenga makubwa yaliyojaa bidhaa na huzunguka mitaani huku wakiuza. Zaidi ya hapo, takriban asilimia 20 ya watu hutumia baisikeli mara moja moja ili kuenda kazini au shuleni. Pia kuna asilimia ndogo ya watu ambao hupanda baisikeli kwa ajili ya mashindano.\n \nMimi ni katika watu walioshindana katika mbio za baisikeli zilizotoka Tanzania hadi Afrika ya Kusini. Sikuwa na nguo zinazotakiwa kwa ajili ya mashindano, kwani sikuwa na uwezo wa kununua mpya kwa sababu muhimu zaidi ilikuwa ni kupata baisikeli haraka. Ilibidi baba aninunulie baisikeli mpya ya mashindano. Ilikuwa ghali sana na alisema hataninunulia baisikeli nyingine kwa miaka kumi ijayo.\n \nTulipofika Afrika ya Kusini nilishangaa kuona barabara maalumu za baisikeli. Niliporudi kwetu nilimhadithia mama yangu aliyewaambia ndugu zetu ‘Salha alipokuwa kule sikuwa na wasiwasi wowote wa ajali za barabarani na sasa mimi nitakwenda naye mwaka ujao’. Mimi nitafurahi kuwa na mama yangu katika mashindano lakini ninahisi nitalazimika kuendesha polepole ili nisimwache nyuma. Yeye ameshanunua taa mpya ambazo amezibandika nyuma na mbele ya baisikeli yake. Pia amenunua mnyororo madhubuti wa kuifungia baisikeli yake ili isiibiwe.\n \nNingefurahia zaidi kama kaka yangu angekubali kuja kwani ni yeye aliyenifundisha kuendesha. Aliwaambia rafiki zake, ‘kamwe sikutegemea kwamba Salha angeenda hadi Afrika ya Kusini kwa baisikeli, safari ndefu na hatari’!",
"grade": "GCSE",
"category": "Reading comprehension"
},
{
"q": "Usaili ulianza saa 4:34 asubuhi na ulimaliza saa 5:50 asubuhi. Jee, usaili ulitumia muda gani?",
"a": "Usaili ulitumia muda wa saa 1 na dakika 16.",
"context": "",
"grade": "4",
"category": "Mathematics"
},
{
"q": "Tatizo kubwa linaloendelea kwa Wambui ni lipi?",
"a": "Wazo la upagazi kuwa kazi ya wanaume",
"context": "Wiki iliyopita nilisoma habari kuhusu Wambui Chege, Mkenya mwenye urefu wa wastani na nywele zilizosokotwa. Yeye ni miongoni mwa wapagazi wachache ambao ni wanawake wanaofanya kazi katika Mlima wa Kilimanjaro uliopo Tanzania. Anapokuwa kazini, yeye huvaa suruali na mabuti mazito.\n\t\t\t\t\t\nShughuli wanazofanya wapagazi ni mojawapo kati ya zile zinazoingiza mamilioni ya fedha ili kukuza uchumi. Pia huduma wanayoitoa huonyesha sura bora ya nchi. Huduma hizi ni kama kuwapa maelfu ya wapandaji milima fursa ya kujishughulisha na zoezi la kupanda mlima bila ya kuwa na wasiwasi kuhusu mizigo yao kwani wapagazi huibeba. Wao ni wenyeji kwa watu wanaopanda milima.\n\t\t\t\t\t\nWapandaji wengi huwa na ufahamu wa kimo kirefu, lakini hushangazwa na kasi ya upepo wa theluji na umati wa watalii wanaokabiliana nao. Wambui anakubaliana nao kwani katika mahojiano yake alisema kwamba mara ya kwanza alipoupanda Mlima wa Kilimanjaro alikata shauri kwamba kamwe asingetaka kurudi tena mlimani huko kutokana na sababu hizo.\n\t\t\t\t\t\nLakini alipopokea mshahara uliokuwa mkubwa kuliko alivyotegemea akaamua kuendelea na kazi hii. Na hadi hivi sasa ameshaupanda mlima huo zaidi ya mara hamsini. Mwanzoni Wambui alichoka sana na hata alishindwa kutembea vizuri kwa maumivu, lakini sasa shida kubwa anayoiona ni ile ya watu wengi kumwambia kwamba upagazi ni shughuli ya wanaume, si ya wanawake. Wao wanahisi kwamba wanawake hawatakiwi kufanya kazi ngumu.\n\t\t\t\t\t\nWambui hakubaliani na mawazo hayo. Alisema kwamba watu wote ni sawa. Yeye kama mpagazi anahitajika zaidi katika maeneo ambayo hayana barabara na anafanya kazi pamoja na wenzake kama waongozaji na wapishi ambao ni wanawake kwa wanaume. Waongozaji ndio viongozi wenyewe na wao hufanya maamuzi yote kuhusu safari. Kwa mfano, huamua muda wa kuanza safari. Wapishi hutayarisha milo pale wasafiri wanapofika katika kambi tofauti. Wambui alifafanua kwamba Mlima wa Kilimanjaro una kambi au vituo vikuu vitatu, navyo ni Mandara, Horombo na Kibo. Wambui alisema kutoka kituo kimoja hadi kingine wapandaji wanaweza kuchukua muda wa saa sita, au hata zaidi wakati wa jua la mchana. Kwa hivyo, mara nyingi waongozaji hufanya uamuzi wa kuukwea mlima gizani, hasa kutokea kituo cha Kibo kuelekea kileleni.\n\t\t\t\t\t\nBaada ya kusikiliza mahojiano ya Wambui nilibaini kwamba kazi wanayofanya wapagazi ndiyo hasa uti wa mgongo wa safari za milimani. Wao hubeba takribani kilo ishirini za vitu muhimu kama mahema, mablanketi, chakula, dawa na maji. Pia hubeba vifaa kama meza, viti na hata magodoro. Hivi sasa Wambui anafanya mafunzo yatakayomwezesha kuwa mwongoza watalii. Hiyo ndiyo ndoto yake. ",
"grade": "GCSE",
"category": "Reading comprehension"
},
{
"q": "Utajumlisha nambari gani na 526 ili jawabu iwe 666?",
"a": "140",
"context": "",
"grade": "4",
"category": "Mathematics"
},
{
"q": "Vijana wa zamani waliwasiliana kwa namna gani? Taja namna mbili.",
"a": "1. Walizungumza ana kwa ana\n2. Waliandikiana barua",
"context": "Wiki iliyopita shule yetu ilitembelewa na Bwana Musa. Yeye ni Mkenya na anafanya utafiti katika chuo kikuu huko Nairobi. Mada ya utafiti wake ni ‘matumizi ya mitandao ya kijamii kwa vijana’. \n\nAlipofika tu, alianza kwa kutuuliza maswali yaliyokuwa na lengo la kuchunguza mienendo na matumizi yetu ya mitandao ya kijamii. Alitaka kujua wanafunzi wangapi huangalia simu zao za mkononi pale wanapoamka tu. Ikabainika kwamba asilimia kubwa kati yetu hufanya hivyo. Wengi wetu hufuatilia picha zinazobandikwa na husoma maoni ya watu tofauti kuhusu picha hizo. Bwana Musa akaongezea kusema kwamba ana uhakika wengi wetu huendelea kuangalia simu zetu za mkononi kila baada ya dakika chache. Hapo tena wanafunzi wengi walicheka huku wakikubaliana na maneno yake. Tena zaidi ya hapo, rafiki yangu Hadija aliongeza ‘ninapoamka tu hukuta nimeshatumiwa ujumbe kama kumi hivi kunitaka nitoe maoni kuhusu picha zilizobandikwa usiku uliopita!’ Hapo tulicheka tena tukikubaliana naye. \n\nBwana Musa alituuliza maswali mengi. Swali ambalo lilinifanya nitafakari kuhusu mambo yanayonivutia linahusu chakula. Aliuliza, ‘wanafunzi wangapi hupiga picha za vyakula kabla ya kuvila?’ Ilibidi ninyooshe kidole na kusema mimi hufanya hivyo. Nilimfahamisha kwamba, pale ninapotembelea mikahawa na kula vyakula vilivyopambwa vizuri, mimi hupendelea kuvipiga picha. Pia hufanya hivyo ninapoviona vyakula ambavyo hupikwa kwa nadra. Siku hizi hata mama yangu haturuhusu kula kabla ya yeye mwenyewe kupiga picha huku akitania ‘hakuna ruhusa ya kula kabla ya kuvipiga picha vyakula’. \n\nBwana Musa alitufahamisha kwamba, maisha tuliyoyazoea sasa ni tofauti kabisa na yale ya watu waliozaliwa miaka kumi au kumi na tano tu iliyopita. Vijana wa sasa hawathamini mazungumzo ya ana kwa ana na hawaandikiani barua kama zamani. Vijana wa sasa wanategemea mitandao ya kijamii ili kuwasiliana na wenzao. Hapo nikaelewa sababu za wazazi wangu kuniambia nipunguze matumizi ya simu. \n\nMimi nimepangiliwa muda maalumu wa kutumia simu ninapokuwa nyumbani. Muda huu ni saa kumi na moja jioni hadi saa kumi na mbili na nusu. Ninamshukuru mama yangu kwa kuupata muda huo ingawa ni mfupi. Baba yangu hapendi kabisa intaneti. Yeye husema ‘ningependelea kama intaneti isingekuwapo kabisa kwani unapotumia intaneti kwa muda mrefu unapoteza ujuzi wako wa kuzungumza kwenye jamii. Pia unajifunza upuuzi na huwi makini darasani kabisa’. \n\nKwa kiasi kikubwa, Bwana Musa alikubaliana na baba yangu kwamba intaneti ni kipingamizi darasani. Lakini alitutahadharisha kwa kusema ‘kuna umuhimu wa kutumia intaneti na mitandao ya kijamii kwani watu hupata ufahamu mkubwa wa mada tofauti na hujenga mahusiano mazuri ya kimataifa’. \n\nAlitupa takwimu chache ambazo zilinishangaza. Kwanza alisema kwamba miaka miwili iliyopita, vijana walitumia takribani saa moja kila siku kwenye mitandao ya kijamii. Pia walikuwa na akaunti moja au mbili tu. Kwa hivyo walitumia muda huo kuangalia mitandao tofauti. Hivi sasa asilimia kubwa ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii ni vijana. Alituuliza, ‘wangapi kati yenu mna uwezo wa kutotazama simu kwa zaidi ya saa zima?’ Hakuna hata mmoja wetu aliyenyoosha kidole. Halafu alituuliza, ‘wangapi kati yenu mna akaunti tano au zaidi kwenye majukwaa tofauti?’ Hapo karibu sote tulinyoosha vidole. Basi Bwana Musa alicheka na kusema, ‘mnaona, nyinyi vijana mnapenda kuwa sehemu tofauti wakati mmoja!’ \n\nMimi ninapotumia intaneti hupenda kusoma hadithi tofauti kwenye tovuti za mitandaoni. Hizi huandikwa na waandishi ambao bado hawajajulikana na huwa nzuri sana. Pia huangalia filamu au vichekesho. \n\nIngawa ninapenda kupiga picha, kwa kawaida hupendelea kubandika picha za vyakula na si picha zinazoonyesha mahala nilipo na familia yangu kwani sitaki kujihatarisha. Bwana Musa alituonya na kusema kwamba, kuna hatia nyingi za kihaini zinazofanyika kwenye mitandao. Alitufahamisha kwamba, kwenye mitandao ya kijamii, vijana hukubali maombi ya urafiki kutoka kwa watu wasiowajua. Mimi sijawahi kufanya hivyo. Alisema kwamba mara nyingi vijana hutazama picha za watu wanaowaomba urafiki na kama zinavutia basi wao hukubali ombi la urafiki. Pia wakati mwingine hutazama kama wana marafiki wa pamoja na hao watu na kukubali urafiki. Kwa hakika uamuzi huu si mzuri kwani, kiukweli, wao hawawajui watu hawa na wanaweza kuwa waovu. Mambo haya huweza kuleta madhara mengi. Mfano ni hatari ya kuibiwa na pia kupoteza usalama kutokana na vitisho tofauti. Bwana Musa alimalizia kwa kututahadharisha wote kwa kusema kwamba ni muhimu kuwa na nidhamu na pia kuwa makini.",
"grade": "GCSE",
"category": "Reading comprehension"
},
{
"q": "Jumla ya wanafunzi 7,500 walifanya mtihani katika kituo chao. Wanafunzi 6,845 walifaulu mtihani huo. Jee, wanafunzi wangapi hawajafaulu mtihani huo?",
"a": "655",
"context": "",
"grade": "4",
"category": "Mathematics"
},
{
"q": "Uwanja wa mpira wa mnazi mmoja una urefu wa mita 800 na upana wa mita 200.Tafuta eneo la uwanja.",
"a": "160,000",
"context": "",
"grade": "4",
"category": "Mathematics"
},
{
"q": "Tofautisha na fananisha maoni ya baba yake mhusika na Bwana Musa kuhusu intaneti. Taja maelezo matano.",
"a": "Baba: kupoteza ujuzi wa kuzungumza kwenye jamii, kujifunza upuuzi.\nMusa: kuwa na ufahamu mkubwa wa mada tofauti, kujenga mahusiano mazuri.\nBaba na Musa: Kutokuwa makini darasani.",
"context": "Wiki iliyopita shule yetu ilitembelewa na Bwana Musa. Yeye ni Mkenya na anafanya utafiti katika chuo kikuu huko Nairobi. Mada ya utafiti wake ni ‘matumizi ya mitandao ya kijamii kwa vijana’. \n\nAlipofika tu, alianza kwa kutuuliza maswali yaliyokuwa na lengo la kuchunguza mienendo na matumizi yetu ya mitandao ya kijamii. Alitaka kujua wanafunzi wangapi huangalia simu zao za mkononi pale wanapoamka tu. Ikabainika kwamba asilimia kubwa kati yetu hufanya hivyo. Wengi wetu hufuatilia picha zinazobandikwa na husoma maoni ya watu tofauti kuhusu picha hizo. Bwana Musa akaongezea kusema kwamba ana uhakika wengi wetu huendelea kuangalia simu zetu za mkononi kila baada ya dakika chache. Hapo tena wanafunzi wengi walicheka huku wakikubaliana na maneno yake. Tena zaidi ya hapo, rafiki yangu Hadija aliongeza ‘ninapoamka tu hukuta nimeshatumiwa ujumbe kama kumi hivi kunitaka nitoe maoni kuhusu picha zilizobandikwa usiku uliopita!’ Hapo tulicheka tena tukikubaliana naye. \n\nBwana Musa alituuliza maswali mengi. Swali ambalo lilinifanya nitafakari kuhusu mambo yanayonivutia linahusu chakula. Aliuliza, ‘wanafunzi wangapi hupiga picha za vyakula kabla ya kuvila?’ Ilibidi ninyooshe kidole na kusema mimi hufanya hivyo. Nilimfahamisha kwamba, pale ninapotembelea mikahawa na kula vyakula vilivyopambwa vizuri, mimi hupendelea kuvipiga picha. Pia hufanya hivyo ninapoviona vyakula ambavyo hupikwa kwa nadra. Siku hizi hata mama yangu haturuhusu kula kabla ya yeye mwenyewe kupiga picha huku akitania ‘hakuna ruhusa ya kula kabla ya kuvipiga picha vyakula’. \n\nBwana Musa alitufahamisha kwamba, maisha tuliyoyazoea sasa ni tofauti kabisa na yale ya watu waliozaliwa miaka kumi au kumi na tano tu iliyopita. Vijana wa sasa hawathamini mazungumzo ya ana kwa ana na hawaandikiani barua kama zamani. Vijana wa sasa wanategemea mitandao ya kijamii ili kuwasiliana na wenzao. Hapo nikaelewa sababu za wazazi wangu kuniambia nipunguze matumizi ya simu. \n\nMimi nimepangiliwa muda maalumu wa kutumia simu ninapokuwa nyumbani. Muda huu ni saa kumi na moja jioni hadi saa kumi na mbili na nusu. Ninamshukuru mama yangu kwa kuupata muda huo ingawa ni mfupi. Baba yangu hapendi kabisa intaneti. Yeye husema ‘ningependelea kama intaneti isingekuwapo kabisa kwani unapotumia intaneti kwa muda mrefu unapoteza ujuzi wako wa kuzungumza kwenye jamii. Pia unajifunza upuuzi na huwi makini darasani kabisa’. \n\nKwa kiasi kikubwa, Bwana Musa alikubaliana na baba yangu kwamba intaneti ni kipingamizi darasani. Lakini alitutahadharisha kwa kusema ‘kuna umuhimu wa kutumia intaneti na mitandao ya kijamii kwani watu hupata ufahamu mkubwa wa mada tofauti na hujenga mahusiano mazuri ya kimataifa’. \n\nAlitupa takwimu chache ambazo zilinishangaza. Kwanza alisema kwamba miaka miwili iliyopita, vijana walitumia takribani saa moja kila siku kwenye mitandao ya kijamii. Pia walikuwa na akaunti moja au mbili tu. Kwa hivyo walitumia muda huo kuangalia mitandao tofauti. Hivi sasa asilimia kubwa ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii ni vijana. Alituuliza, ‘wangapi kati yenu mna uwezo wa kutotazama simu kwa zaidi ya saa zima?’ Hakuna hata mmoja wetu aliyenyoosha kidole. Halafu alituuliza, ‘wangapi kati yenu mna akaunti tano au zaidi kwenye majukwaa tofauti?’ Hapo karibu sote tulinyoosha vidole. Basi Bwana Musa alicheka na kusema, ‘mnaona, nyinyi vijana mnapenda kuwa sehemu tofauti wakati mmoja!’ \n\nMimi ninapotumia intaneti hupenda kusoma hadithi tofauti kwenye tovuti za mitandaoni. Hizi huandikwa na waandishi ambao bado hawajajulikana na huwa nzuri sana. Pia huangalia filamu au vichekesho. \n\nIngawa ninapenda kupiga picha, kwa kawaida hupendelea kubandika picha za vyakula na si picha zinazoonyesha mahala nilipo na familia yangu kwani sitaki kujihatarisha. Bwana Musa alituonya na kusema kwamba, kuna hatia nyingi za kihaini zinazofanyika kwenye mitandao. Alitufahamisha kwamba, kwenye mitandao ya kijamii, vijana hukubali maombi ya urafiki kutoka kwa watu wasiowajua. Mimi sijawahi kufanya hivyo. Alisema kwamba mara nyingi vijana hutazama picha za watu wanaowaomba urafiki na kama zinavutia basi wao hukubali ombi la urafiki. Pia wakati mwingine hutazama kama wana marafiki wa pamoja na hao watu na kukubali urafiki. Kwa hakika uamuzi huu si mzuri kwani, kiukweli, wao hawawajui watu hawa na wanaweza kuwa waovu. Mambo haya huweza kuleta madhara mengi. Mfano ni hatari ya kuibiwa na pia kupoteza usalama kutokana na vitisho tofauti. Bwana Musa alimalizia kwa kututahadharisha wote kwa kusema kwamba ni muhimu kuwa na nidhamu na pia kuwa makini.",
"grade": "GCSE",
"category": "Reading comprehension"
},
{
"q": "Tunajuaje kwamba mwandishi anathamini kazi ya Wambui?",
"a": "Anasema kazi yake ni ‘uti wa mgongo’",
"context": "Wiki iliyopita nilisoma habari kuhusu Wambui Chege, Mkenya mwenye urefu wa wastani na nywele zilizosokotwa. Yeye ni miongoni mwa wapagazi wachache ambao ni wanawake wanaofanya kazi katika Mlima wa Kilimanjaro uliopo Tanzania. Anapokuwa kazini, yeye huvaa suruali na mabuti mazito.\n\t\t\t\t\t\nShughuli wanazofanya wapagazi ni mojawapo kati ya zile zinazoingiza mamilioni ya fedha ili kukuza uchumi. Pia huduma wanayoitoa huonyesha sura bora ya nchi. Huduma hizi ni kama kuwapa maelfu ya wapandaji milima fursa ya kujishughulisha na zoezi la kupanda mlima bila ya kuwa na wasiwasi kuhusu mizigo yao kwani wapagazi huibeba. Wao ni wenyeji kwa watu wanaopanda milima.\n\t\t\t\t\t\nWapandaji wengi huwa na ufahamu wa kimo kirefu, lakini hushangazwa na kasi ya upepo wa theluji na umati wa watalii wanaokabiliana nao. Wambui anakubaliana nao kwani katika mahojiano yake alisema kwamba mara ya kwanza alipoupanda Mlima wa Kilimanjaro alikata shauri kwamba kamwe asingetaka kurudi tena mlimani huko kutokana na sababu hizo.\n\t\t\t\t\t\nLakini alipopokea mshahara uliokuwa mkubwa kuliko alivyotegemea akaamua kuendelea na kazi hii. Na hadi hivi sasa ameshaupanda mlima huo zaidi ya mara hamsini. Mwanzoni Wambui alichoka sana na hata alishindwa kutembea vizuri kwa maumivu, lakini sasa shida kubwa anayoiona ni ile ya watu wengi kumwambia kwamba upagazi ni shughuli ya wanaume, si ya wanawake. Wao wanahisi kwamba wanawake hawatakiwi kufanya kazi ngumu.\n\t\t\t\t\t\nWambui hakubaliani na mawazo hayo. Alisema kwamba watu wote ni sawa. Yeye kama mpagazi anahitajika zaidi katika maeneo ambayo hayana barabara na anafanya kazi pamoja na wenzake kama waongozaji na wapishi ambao ni wanawake kwa wanaume. Waongozaji ndio viongozi wenyewe na wao hufanya maamuzi yote kuhusu safari. Kwa mfano, huamua muda wa kuanza safari. Wapishi hutayarisha milo pale wasafiri wanapofika katika kambi tofauti. Wambui alifafanua kwamba Mlima wa Kilimanjaro una kambi au vituo vikuu vitatu, navyo ni Mandara, Horombo na Kibo. Wambui alisema kutoka kituo kimoja hadi kingine wapandaji wanaweza kuchukua muda wa saa sita, au hata zaidi wakati wa jua la mchana. Kwa hivyo, mara nyingi waongozaji hufanya uamuzi wa kuukwea mlima gizani, hasa kutokea kituo cha Kibo kuelekea kileleni.\n\t\t\t\t\t\nBaada ya kusikiliza mahojiano ya Wambui nilibaini kwamba kazi wanayofanya wapagazi ndiyo hasa uti wa mgongo wa safari za milimani. Wao hubeba takribani kilo ishirini za vitu muhimu kama mahema, mablanketi, chakula, dawa na maji. Pia hubeba vifaa kama meza, viti na hata magodoro. Hivi sasa Wambui anafanya mafunzo yatakayomwezesha kuwa mwongoza watalii. Hiyo ndiyo ndoto yake. ",
"grade": "GCSE",
"category": "Reading comprehension"
},
{
"q": "Chukua 450 kutoka 742, jawabu yake ni:",
"a": "292",
"context": "",
"grade": "4",
"category": "Mathematics"
},
{
"q": "Ikiwa kilo moja ya sukari inauzwa shilingi 2000. Jee, kilo 9 zitauzwa kwa shilingi ngapi?",
"a": "18000",
"context": "",
"grade": "4",
"category": "Mathematics"
},
{
"q": "Fikra za walimu kuhusu jinsi ya kushughulikia matumizi ya simu darasani.",
"a": "[\"Kuhakikisha kwamba haileti fujo darasani\", \"kusaidia wanafunzi kutumia simu vizuri\"]",
"context": "Kweli wanafunzi wa leo ni wenyeji wa enzi za kiteknolojia. Kulingana na utafiti uliochapishwa mwaka uliopita, vijana watatu kati ya wanne siku hizi wana simu za kisasa na wengi wanazileta shuleni kila siku. Lakini je, ni wazo zuri kuwaruhusu wanafunzi walete au watumie simu zao darasani? Tulizungumza na walimu, wanafunzi na wazazi kufahamu zaidi.\n \nFarouk ni mwalimu wa hesabu katika shule ya kimataifa Kampala. Alianza kufundisha miaka kumi iliyopita, wakati ambapo hakukuwa na wanafunzi wo wote wenye simu. Anaona kwamba simu zinaweza kuwasaidia walimu, kwa mfano kusambaza taarifa na kuwatumia wanafunzi mazoezi ya kazi za nyumbani. Lakini anataka wanafunzi wasiruhusiwe kabisa kuzileta darasani. ‘Kwangu, simu darasani ni hatari tu. Kwanza, zinawawezesha wanafunzi kuibia katika mitihani, na kweli tatizo hili limeenea sana hivi sasa. Pia wanafunzi wenye simu hawasikilizi darasani na hukengeushwa nazo mara nyingi. Darasani ni kazi ya wanafunzi kusikiliza na kusoma, na ni kazi ya mwalimu kuhakikisha kwamba hakuna fujo. Kwa maoni yangu simu ni kipingamizi tu.’\n \nKhadija na Jonathan wanaishi Moshi na ni rafiki wa miaka mingi. Wote wawili wanasoma kwenye shule moja ya sekondari Moshi. Jonathan ana miaka kumi na mitano, na anapenda sana masomo ya sanaa. Hakubali kwamba matumizi ya simu za mikononi huleta shida darasani, bali anafikiri shida ni walimu wasiojaribu kufanya madarasa yawapendeze wanafunzi. ‘Ninampenda sana mwalimu wangu wa sanaa – madarasa yake ni ya kuvutia na sina haja ya kuangalia simu yangu. Lakini walimu wengine wanaongea tu na ni vigumu kukaa na kusikiliza kwa masaa mengi mfululizo.’\n \nKhadija anacheka na kuzungusha macho kwa mzaha. Yeye ni msichana mwenye umri wa miaka kumi na minne, na ni mwanafunzi hodari aliyetunukiwa Tuzo la Darasa mwaka uliopita. Mama yake alimnunulia simu kama zawadi kwa kupata Tuzo hilo. Khadija anakubali si shida kubwa kutumia simu darasani, lakini bora uzitumie kusaidia ufahamu wako – sio kujikengeusha tu. ‘Simu yangu ya kisasa inanisaidia kupata majibu kwa urahisi zaidi. Sasa sihitaji kumwuliza mwalimu maswali na ninaweza kufahamu zaidi muktadha wa mada zinazofundishwa. Kwa mfano, juzi tulikuwa tukisoma kuhusu Azimio la Arusha na niliweza kupitia makala na magazeti pale pale nilipokaa darasani!’\n \nMama Khadija alikuwa na hofu kidogo alipomnunulia mtoto wake simu, kwa sababu wazazi wengi walikuwa wamemlalamikia kuhusu athari za simu za kisasa kwa watoto wao. ‘Wengi waliniambia kwamba alama zao zilishuka mno. Wanalalamika kwamba watoto wao hawataki kufanya kazi zao za nyumbani, bali wanapendelea kutumia masaa kwenye mitandao ya kijamii au kucheza michezo ya simuni tu.’ Lakini anasema bado hajaona athari mbaya kwa Khadija. ‘Alama zake bado ni za juu, na hutumia simu yake kusambaza taarifa kati yake na rafiki zake kwenye vikundi vyao vya masomo ya shule. Pia sasa simu ni sehemu ya maisha tu na usipoweza kuzitumia utapitwa na wakati. Sijamwekea masharti yo yote, na nimeona ameitumia kwa makini.’ Khadija anatabasamu na kuongeza: ‘Kwa kweli, nilishukuru jinsi mamangu alivyoniamini na nilitaka kumthibitishia kwamba alikuwa sahihi. Kwa hivyo, nimekuwa nikitumia simu kwa uangalifu.’\n \nMwalimu Ida Hamdani alianza kufundisha miezi sita iliyopita. Yeye hakutaka kupiga marufuku simu darasani. Bali, amegundua kwamba simu zinaweza kuwa chombo cha kuboresha mazingira ya masomo darasani kwa wanafunzi na walimu pia, mradi tu unasimamia jinsi zinavyotumiwa. Kwake, hali halisi ni kwamba vijana hutumia simu kila siku, tena watapaswa kuzitumia katika maisha yao yajayo, na ni wajibu wa walimu kuwasaidia kuzitumia kwa njia sahihi. ‘Kitu cha muhimu ni kuweka sheria kwa matumizi ya simu darasani, pamoja na kueleza wazi wanafunzi watakavyoathirika zikitumiwa vibaya. Ukijaribu kuwazuia wanafunzi wasitumie simu kabisa, wataasi tu, lakini ukishirikiana nao kuhakikisha kwamba wanazitumia kwa njia nzuri, watakubali.’",
"grade": "GCSE",
"category": "Reading comprehension"
},
{
"q": "Bwana Ali alitoa mchele kilogramu 1000 kwa familia zilizopo kijijini. Ikiwa kila familia moja ilipata kilogramu 20. Jee, familia ngapi zilifaidika na mchango huo?",
"a": "50",
"context": "",
"grade": "4",
"category": "Mathematics"
},
{
"q": "Kijiji kilikuwa kinafanya matendo gani ambayo ni mabaya kwa mazingira? Taja matendo mawili.",
"a": "[\"Kutumia majiko yenye uchafuzi [ya kuni/mkaa]\", \"Kukata miti [bila kudhibiti]\"]",
"context": "",
"grade": "GCSE",
"category": "Reading comprehension"
},
{
"q": "Nyumba ya bwana Ali ilikua na urefu wa sentimita 3000. Jee, nyumba hiyo itakua na urefu wa mita ngapi?",
"a": "30",
"context": "",
"grade": "4",
"category": "Mathematics"
},
{
"q": "Kwa nini Salha angependelea kuingia kwenye mashindano na kaka na si mama? Taja sababu mbili.",
"a": "[\"Mama anaendesha polepole\", \"Kaka alimfundisha kuendesha\"]",
"context": "Kuna aina nyingi za usafiri wa kila siku. Mtu anaweza kuendesha gari, kupanda basi au treni, kukodi teksi au kutembea kwa miguu. Inaonekana kwamba siku hizi watu wengi wanapenda sana kutembea au kupanda baisikeli. Zamani watu walipopanda baisikeli au kutembea walionekana kama fukara na hawana uwezo wa kununua gari au kulipia usafiri wa umma. Siku hizi watu wanaelewa kuwa magari yanaleta uchafuzi wa mazingira, na pia kuna sababu za kiuchumi kwani kutembea na kutumia baisikeli ni bure kabisa. Hata hivyo huku kwetu bado gari linaendelea kuwa muhimu kwani watu wengine huwa na familia kubwa inayojumuisha ndugu na jamaa tofauti, kwa hivyo ni lazima kuwa na usafiri madhubuti.\n \nNilifanya utafiti pamoja na kaka yangu na tuligundua kwamba katika mji wetu, zaidi ya asilimia 50 ya watu hutumia baisikeli kama njia yao kuu ya usafiri. Kati ya hawa, wapo ambao hufanyia kazi zao kwenye baisikeli. Mfano mzuri ni wale wanaouza madafu, mboga na matunda ambayo huyapakia kwenye baisikeli zao. Wao huwa na matenga makubwa yaliyojaa bidhaa na huzunguka mitaani huku wakiuza. Zaidi ya hapo, takriban asilimia 20 ya watu hutumia baisikeli mara moja moja ili kuenda kazini au shuleni. Pia kuna asilimia ndogo ya watu ambao hupanda baisikeli kwa ajili ya mashindano.\n \nMimi ni katika watu walioshindana katika mbio za baisikeli zilizotoka Tanzania hadi Afrika ya Kusini. Sikuwa na nguo zinazotakiwa kwa ajili ya mashindano, kwani sikuwa na uwezo wa kununua mpya kwa sababu muhimu zaidi ilikuwa ni kupata baisikeli haraka. Ilibidi baba aninunulie baisikeli mpya ya mashindano. Ilikuwa ghali sana na alisema hataninunulia baisikeli nyingine kwa miaka kumi ijayo.\n \nTulipofika Afrika ya Kusini nilishangaa kuona barabara maalumu za baisikeli. Niliporudi kwetu nilimhadithia mama yangu aliyewaambia ndugu zetu ‘Salha alipokuwa kule sikuwa na wasiwasi wowote wa ajali za barabarani na sasa mimi nitakwenda naye mwaka ujao’. Mimi nitafurahi kuwa na mama yangu katika mashindano lakini ninahisi nitalazimika kuendesha polepole ili nisimwache nyuma. Yeye ameshanunua taa mpya ambazo amezibandika nyuma na mbele ya baisikeli yake. Pia amenunua mnyororo madhubuti wa kuifungia baisikeli yake ili isiibiwe.\n \nNingefurahia zaidi kama kaka yangu angekubali kuja kwani ni yeye aliyenifundisha kuendesha. Aliwaambia rafiki zake, ‘kamwe sikutegemea kwamba Salha angeenda hadi Afrika ya Kusini kwa baisikeli, safari ndefu na hatari’!",
"grade": "GCSE",
"category": "Reading comprehension"
},
{
"q": "Unajuaje kwamba uchumi una nafasi kubwa kwenye utalii wa anga?",
"a": "[\"Watu wanaojiweza kifedha wataweza kuenda angani\", \"Tofauti kati ya watu duniani zitazidi kuwa kubwa/matabaka\", \"Mamilioni hutumika kuenda angani / Wadau kuwekeza fedha kwenye miradi ya angani\", \"Mafuta mengi yenye thamani ya juu\"]",
"context": "",
"grade": "GCSE",
"category": "Reading comprehension"
},
{
"q": "Andika majina ya miezi yenye siku thelathini.",
"a": "Aprili, Juni, Septemba, Novemba",
"context": "",
"grade": "Maths",
"category": "Reading comprehension"
},
{
"q": "Jambo gani lilimfanya Vanessa aanze kutambulika kama mwanaharakati?",
"a": "Kuandamana/Maandamano",
"context": "",
"grade": "GCSE",
"category": "Reading comprehension"
},
{
"q": "Kwa nini waongozaji huanza safari wakati wa usiku?",
"a": "Kuokoa muda/kufika kwa haraka zaidi",
"context": "Wiki iliyopita nilisoma habari kuhusu Wambui Chege, Mkenya mwenye urefu wa wastani na nywele zilizosokotwa. Yeye ni miongoni mwa wapagazi wachache ambao ni wanawake wanaofanya kazi katika Mlima wa Kilimanjaro uliopo Tanzania. Anapokuwa kazini, yeye huvaa suruali na mabuti mazito.\n\t\t\t\t\t\nShughuli wanazofanya wapagazi ni mojawapo kati ya zile zinazoingiza mamilioni ya fedha ili kukuza uchumi. Pia huduma wanayoitoa huonyesha sura bora ya nchi. Huduma hizi ni kama kuwapa maelfu ya wapandaji milima fursa ya kujishughulisha na zoezi la kupanda mlima bila ya kuwa na wasiwasi kuhusu mizigo yao kwani wapagazi huibeba. Wao ni wenyeji kwa watu wanaopanda milima.\n\t\t\t\t\t\nWapandaji wengi huwa na ufahamu wa kimo kirefu, lakini hushangazwa na kasi ya upepo wa theluji na umati wa watalii wanaokabiliana nao. Wambui anakubaliana nao kwani katika mahojiano yake alisema kwamba mara ya kwanza alipoupanda Mlima wa Kilimanjaro alikata shauri kwamba kamwe asingetaka kurudi tena mlimani huko kutokana na sababu hizo.\n\t\t\t\t\t\nLakini alipopokea mshahara uliokuwa mkubwa kuliko alivyotegemea akaamua kuendelea na kazi hii. Na hadi hivi sasa ameshaupanda mlima huo zaidi ya mara hamsini. Mwanzoni Wambui alichoka sana na hata alishindwa kutembea vizuri kwa maumivu, lakini sasa shida kubwa anayoiona ni ile ya watu wengi kumwambia kwamba upagazi ni shughuli ya wanaume, si ya wanawake. Wao wanahisi kwamba wanawake hawatakiwi kufanya kazi ngumu.\n\t\t\t\t\t\nWambui hakubaliani na mawazo hayo. Alisema kwamba watu wote ni sawa. Yeye kama mpagazi anahitajika zaidi katika maeneo ambayo hayana barabara na anafanya kazi pamoja na wenzake kama waongozaji na wapishi ambao ni wanawake kwa wanaume. Waongozaji ndio viongozi wenyewe na wao hufanya maamuzi yote kuhusu safari. Kwa mfano, huamua muda wa kuanza safari. Wapishi hutayarisha milo pale wasafiri wanapofika katika kambi tofauti. Wambui alifafanua kwamba Mlima wa Kilimanjaro una kambi au vituo vikuu vitatu, navyo ni Mandara, Horombo na Kibo. Wambui alisema kutoka kituo kimoja hadi kingine wapandaji wanaweza kuchukua muda wa saa sita, au hata zaidi wakati wa jua la mchana. Kwa hivyo, mara nyingi waongozaji hufanya uamuzi wa kuukwea mlima gizani, hasa kutokea kituo cha Kibo kuelekea kileleni.\n\t\t\t\t\t\nBaada ya kusikiliza mahojiano ya Wambui nilibaini kwamba kazi wanayofanya wapagazi ndiyo hasa uti wa mgongo wa safari za milimani. Wao hubeba takribani kilo ishirini za vitu muhimu kama mahema, mablanketi, chakula, dawa na maji. Pia hubeba vifaa kama meza, viti na hata magodoro. Hivi sasa Wambui anafanya mafunzo yatakayomwezesha kuwa mwongoza watalii. Hiyo ndiyo ndoto yake. ",
"grade": "GCSE",
"category": "Reading comprehension"
},
{
"q": "Mabadiliko ya vitendo vya wenyeji tofauti kuhusu ndege zisizo na rubani:",
"a": "[\"Hawataki kuingia porini\", \"Wengine wanazidungua/wanaziharibu\", \"Wakulima wengine wamezikubali\", \"Wanaishi kwa hofu\"]",
"context": "",
"grade": "GCSE",
"category": "Reading comprehension"
},
{
"q": "Kwa nini watu wanaendesha baisikeli sasa? Taja sababu mbili.",
"a": "[\"mazingira\", \"uchumi (bure)\"]",

}
]