_id
stringlengths 15
22
| url
stringlengths 31
150
| title
stringlengths 1
86
| text
stringlengths 100
23.8k
|
---|---|---|---|
20231101.sw_1676_43
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Kutiwa mbaroni kwa Warũhiũ Itote (aka General China) tarehe 15 Januari 1954, na kuhojiwa kwake kulipelekea Waingereza kuuelewa vyema usimamizi wa Mau Mau. Oparesheni Anvil iliyoanzishwa tarehe 24 Aprili 1954 ilipangwa na jeshi kwa wiki kadhaa baada ya kukubaliwa na kamati kuu ya vita. Wakati wa oparesheni hiyo, mji wa Nairobi ulidhibitiwa na wanajeshi na wakazi wake walihojiwa huku wafuasi wa Mau Mau wakikamatwa na kupelekwa vizuizini.
|
20231101.sw_1676_44
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Mnamo Mei 1953, walinzi wa nyumbani walitambulika rasmi kama askari wa usalama. Askari hao wa nyumbani ndio waliounda kikosi cha kupambana na mikakati ya Mau Mau kwani walikuwa Waafrika waaminifu, na si majeshi ya kigeni kama Jeshi la Uingereza na King's African Rifles. Kufikia mwisho wa hali ya hatari, askari hao walikuwa wamewaua Mau Mau 4886, ambao ni asilimia 42% ya waasi wote. Kukamatwa kwa Dedan Kimathi huko Nyeri tarehe 21 Oktoba 1956 kuliashiria kushindwa kwa Mau Mau kukamaliza vita.
|
20231101.sw_1676_45
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Waafrika walichaguliwa moja kwa moja katika bunge la uwakilishi kwa mara ya kwanza mwaka wa 1957. Licha ya Waingereza kutamani kuwakabidhi mamlaka wapinzani wasio na siasa kali ya Kiafrika, ni chama cha Kenya African National Union (KANU) kilichoongozwa na Jomo Kenyatta kilichounda serikali punde tu kabla ya Kenya kupata uhuru tarehe 12 Desemba 1963. Tarehe 12 Desemba 1964, Kenya ilipotangazwa kuwa jamhuri, Kenyatta akawa rais wa kwanza.
|
20231101.sw_1676_46
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Mwaka huohuo, jeshi la Kenya lilipigana na Vita vya Shifta dhidi ya kabila la Wasomali waliokusudia kuiona NFD imejiunga na Jamhuri ya Somalia. Mashifta walililemea jeshi la Kenya lakini baadaye walishindwa mwaka wa 1967.
|
20231101.sw_1676_47
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Kenya ilitia saini mkataba na nchi ya Ethiopia mwaka wa 1969 unaodumu mpaka leo kwa kuhofia mashambulizi kutoka kwa jeshi la Somalia lililokuwa na nguvu zaidi. Eneo la NFD nchini Kenya halijaendelea kutokana na kiangazi na mafuriko. Hata hivyo, wakimbizi wafanyabiashara wa Kisomali waliotajirika wamebadilisha mtaa wa Eastleigh uliokuwa wa mabanda na kuufanya kuwa ngome ya kibiashara katika sehemu kubwa ya mashariki mwa mji wa Nairobi.
|
20231101.sw_1676_48
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Mwaka wa 1978, Kenyatta alifariki na Daniel Arap Moi akawa rais. Moi alidumisha urais kwa kuchaguliwa bila kupingwa katika chaguzi za mwaka wa 1979, 1983 (uchaguzi wa dharura) na 1988, zote zikiwa zilifanyika chini ya katiba ya chama kimoja. Uchaguzi wa 1983 ulifanyika mwaka mmoja kabla ya wakati kutokana na njama ya kupindua serikali iliyokosa kufaulu tarehe 1 Agosti 1982.
|
20231101.sw_1676_49
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Mapinduzi hayo yaliyotibuka yalipangwa na askari mwanahewa wa cheo cha chini, Bwana Hezekiah Ochuka na kuendelezwa hasa na wanahewa. Jaribio hilo lilizimwa kwa haraka na wanajeshi waaminifu wakiongozwa na Jeshi la Nchi Kavu, General Service Unit (GSU) - kikosi cha polisi wenye hadhi ya kijeshi - na baadaye polisi wa kawaida. Hata hivyo raia kadhaa walijeruhiwa na wengine kuuawa. Tukio hilo lilisababisha kuvunjwa kwa kikosi chote cha wanahewa, huku wengine wakiachishwa kazi na wengine wakishtakiwa kwenye mahakama ya kijeshi.
|
20231101.sw_1676_50
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Katika uchaguzi wa 1988 kura za mlolongo zilianzishwa, ambapo wapigakura walitakiwa kupiga foleni nyuma ya wagombea wanaowapenda, badala ya kutumia kura ya siri Jambo hilo lilionekana kama kilele cha enzi ya ukiukaji mkubwa wa demokrasia likasababisha msukumo mkuu wa mageuzi ya kikatiba. Vipengele vilivyokuwa na utata, kikiwemo kile kilichoruhusu chama kimoja pekee cha kisiasa, vilibadilishwa miaka iliyofuata.
|
20231101.sw_1676_51
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Katika uchaguzi wa kidemokrasia wa vyama vingi wa miaka ya 1992 na 1997, Daniel Arap Moi alichaguliwa tena.
|
20231101.sw_1676_52
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Kulingana na katiba, mwaka 2002 Moi hakuruhusiwa kuwania urais tena, na Mwai Kibaki wa chama cha upinzani cha "National Rainbow Coalition" — NARC akachaguliwa kuwa rais. Uchaguzi huo ulitambulikana kuwa wa kidemokrasia na wachunguzi wa humu nchini na wa kimataifa na hivyo kuwa chanzo cha mageuzi makubwa ya kidemokrasia nchini Kenya.
|
20231101.sw_1676_53
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Mnamo Desemba 2002, Wakenya walifanya uchaguzi uliokuwa wa kidemokrasia na uwazi ambao kwa kiasi kikubwa uliamuliwa kuwa huru na wa haki na wachunguzi wa kimataifa. Uchaguzi wa mwaka huo ulikuwa mwanzo mpya na uliiletea Kenya mabadiliko makuu ya kisiasa yaliyowezesha chama cha Kenya African National Union (KANU), kilichokuwa kimeitawala nchi tangu uhuru, kukabidhi kwa amani mamlaka kwa chama cha National Rainbow Coalition (NARK), uliokuwa muungano wa vyama vingi.
|
20231101.sw_1676_54
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Chini ya uongozi wa Rais Mwai Kibaki, muungano wa vyama tawala ulihahidi kushughulikia ukuaji wa kiuchumi, kumaliza ufisadi, kuimarisha elimu na kuandika katiba mpya. Baadhi ya ahadi hizi zimeshatimizwa. Kuna elimu ya msingi ya bure. Mwaka wa 2007 serikali ilitangaza kuwa, kuanzia mwaka 2008 gharama ya masomo ya shule za upili itapunguzwa huku serikali ikilipia gharama zote za mafundisho.
|
20231101.sw_1676_55
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 27 Desemba 2007, Rais Kibaki wa chama cha Party of National Unity (PNU) aliwania uchaguzi dhidi ya chama kikuu cha upinzani Orange Democratic Movement (ODM). Kulingana na wachunguzi wa kimataifa, uchaguzi huo ulikumbwa na udanganyifu na hivyo kutofikia kiwango kinachokubalika kimataifa. Chama cha ODM kilisambaratika na kupoteza 8 % ya kura zake kwa chama kipya cha Orange Democratic Movement-Kenya (ODM) - kikiongozwa na Kalonzo Musyoka. Kinyang’anyiro kilikuwa kikali kati ya mgombea wa ODM, Raila Odinga na Kibaki wa PNU. Kuhesabiwa kwa kura na Tume ya Uchaguzi ya Kenya kulionyesha Raila akiongoza kwa kura chache na baadaye kwa kura nyingi. Hata hivyo, kura zilipoendelea kuhesabiwa na Tume ya Uchaguzi, Kibaki alimkaribia mpinzani wake kwa kura, kisha akamshinda. Matokeo hayo yalisababisha maandamano na kulaumiwa kwa Tume ya Uchaguzi ya Kenya kwa kumpendelea Kibaki, hivyo Oginga akajitangaza “rais wa watu” na kutaka kura zihesabiwe tena.
|
20231101.sw_1676_56
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Maandamano hayo yalibadilika kuwa ghasia zilizosababisha kuharibiwa kwa mali.. Viongozi mashuhuri wa Afrika, wakiongozwa na aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan walisuluhisha mzozo huo wa kisiasa. Kundi la Annan liliungwa mkono na Umoja wa Mataifa, Jumuia ya Ulaya, Muungano wa Nchi za Afrika, Serikali ya Marekani na nchi nyingine maarufu ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi rejelea Ghasia nchini Kenya (2007-2008).
|
20231101.sw_1676_57
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Annan aliomba usaidizi kwa kamati yake ya upatanishi kutoka kwa shirika la kushughulikia mizozo la Uswisi lijulikanalo kama Kituo cha Mazungumzo ya Kihisani yaani Centre for Humanitarian Dialogue.
|
20231101.sw_1676_58
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Tarehe 12 Februari 2008 Kibaki na Odinga walitia sahihi mkataba wa kuunda serikali ya muungano ambapo Odinga angekuwa waziri mkuu wa pili nchini Kenya. Kulingana na mkataba huo, rais angeteua baraza la mawaziri kutoka pande zote mbili za PNU na ODM kulingana na wingi wa wabunge wa kila chama bungeni. Mkataba huo ulieleza kuwa baraza la mawaziri litajumuisha Makamu wa Rais na manaibu wawili wa Waziri Mkuu. Baada ya majadiliano bungeni ilipitishwa kuwa muungano huo utadumu hadi mwisho wa kipindi cha bunge, ama chama kimoja kikijitoa kwenye muungano kabla ya kipindi cha bunge kuisha.
|
20231101.sw_1676_59
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Wadhifa huo mpya wa waziri mkuu utakuwa na nguvu na mamlaka kuratibu na kusimamia shughuli za serikali. Vilevile itaongozwa na mbunge aliyechaguliwa ambaye pia atakuwa kiongozi wa chama au muungano wa vyama wenye idadi kubwa ya wabunge bungeni. Ulimwengu ulimshuhudia Annan na kamati yake iliyoungwa mkono na Umoja wa Mataifa na mwenye kiti wa muungano wa nchi za Afrika Jakaya Kikwete, walipowaleta pamoja wapinzani hawa sugu kwenye sherehe za kutia sahihi mkataba huu. Sherehe hizi zilionyeshwa moja kwa moja kwenya televisheni ya kitaifa kutoka kiingilio cha Jumba la Harambee mjini Nairobi. Wawakilishi wa PNU na ODM walianza majadiliano ya kina kuhusu ugavi wa mamlaka tarehe 29 Februari 2008. Wabunge wa Kenya, kwa pamoja, waliidhinisha mkataba wa ugawaji mamlaka tarehe 18 mwezi wa Machi 2008 ili kuiokoa Kenya iliyoaminika kama mojawapo ya nchi thabiti na iliyoendelea barani Afrika. Mkataba huu uliunganisha PNU iliyoongozwa na Kibaki na ODM ya Odinga kisha kupelekea kuundwa kwa serikali ya muungano, vyama vyote viwili vikiwa na mamlaka sawa.
|
20231101.sw_1676_60
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Tarehe 13 Aprili 2008, Rais Kibaki aliitangaza baraza la mawaziri 41 wa serikali hii ya muungano ikijumuisha waziri mkuu na makamu wake wawili. Baraza hili lilijumuisha pia manaibu wa mawaziri 50 na lilitawazwa katika Ikulu ya Nairobi tarehe 17 Aprili 2008 huku Kofi Annan na viongozi wengine mashuhuri wakishuhudia.
|
20231101.sw_1676_61
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Tarehe 4 Novemba 2008 ilitangazwa kuwa sikukuu ya kitaifa kusherehekea ushindi wa Barack Obama, ambaye baba yake alikuwa Mkenya, kama rais wa Marekani.
|
20231101.sw_1676_62
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Katika sehemu za mashambani, kama wilayani Kisii, visa vya kuchoma watu wakidaiwa kuwa wachawi vinaongezeka. Waathiriwa hasa ni wanawake wakongwe. Mnamo Mei 2008, watu 11 waliuwa na nyumba 30 kuchomwa.
|
20231101.sw_1676_63
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Kwa sasa Kenya ni jamhuri ya kidemokrasia ya kiuwakilishi inayoongozwa na rais, ambaye ndiye mkuu wa taifa na kiongozi wa serikali, na yenye mfumo wa vyama vingi. Serikali ndiyo yenye mamlaka ya juu.
|
20231101.sw_1676_64
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Utungaji wa sheria ni jukumu la serikali na la bunge la taifa. Idara ya Mahakama ni huru, na imejitenga na serikali kuu na bunge. Hata hivyo, kulikuwa na kutoridhika kwingi, hasa katika enzi ya rais mstaafu Daniel Arap Moi, kuwa serikali iliingilia sana shughuli za mahakama.
|
20231101.sw_1676_65
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Kenya imedumisha uthabiti wa kutosha licha ya mabadiliko katika mifumo yake ya kisiasa na michafuko katika nchi kadhaa jirani. Bunge la mseto wa vyama vingi la 1997 lilianzisha mageuzi yaliyobadilisha sheria za kikoloni zenye dhuluma zilizotumika kuuzuia uhuru wa kuongea na kutangamana. Jambo hilo liliimarisha uhuru wa umma na kuchangia kiasi kuaminika kwa uchaguzi wa Desemba 1997.
|
20231101.sw_1676_66
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Kenya ina kaunti 47, kila moja ikiongozwa na Mkuu wa Kaunti anayechaguliwa na watu ambao wanaishi kwenye hiyo kaunti.
|
20231101.sw_1676_67
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Serikali za mitaa huendelezwa kupitia mabaraza ya miji. Maeneo mengi ya mijini huwa ni mji, manisipaa au baraza la mji. Serikali za mitaa katika maeneo ya mashambani huitwa serikali za wilaya. Madiwani wa mitaa hii huchaguliwa katika uchaguzi wa madiwani unaofanywa wakati mmoja na uchaguzi mkuu.
|
20231101.sw_1676_68
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Maeneo ya uwakilishi bungeni yamegawanywa kwa sababu ya upigaji kura. Kuna maeneobunge 210 nchini Kenya.
|
20231101.sw_1676_69
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Kenya ni nchi yenye makabila mengi tofautitofauti, hasa ya Kibantu (67%) na ya Kiniloti. Wakenya wengi huzungumza lugha mbili, Kiingereza na Kiswahili, na asilimia kubwa pia huzungumza lugha mama ya kabila lao.
|
20231101.sw_1676_70
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Makundi ya makabila ni kama ifuatavyo: Wakikuyu 22%, Waluyia 14%, Wajaluo 13%, Wakalenjin 12%, Wakamba 11%, Wakisii 6%, Wameru 6%, makabila mengine ya Kiafrika 15%, wasio Waafrika (Wahindi, Waingereza na Waarabu) 1%
|
20231101.sw_1676_71
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Kila kundi au kabila lina lugha yake na Kiswahili hutumika kama chombo cha kuwasiliana miongoni mwa makabila tofauti.
|
20231101.sw_1676_72
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Upande wa dini, idadi kubwa ya Wakenya ni Wakristo: kulingana na sensa ya mwaka 2019, asilimia 85.5 ya wakazi wa Kenya walikuwa Wakristo (asilimia 53.9 ni Waprotestanti, asilimia 20.6 ni Wakatoliki, asilimia 11.8 ni Wakristo wa madhehebu mengine mbalimbali, wakiwemo Waorthodoksi 621,200), asilimia 10.9 ni Waislamu, asilimia 0.7 ni wafuasi wa dini asilia za Kiafrika, asilimia 1.7 ni wa makundi mengine ya dini (kuna Wahindu takribani 60,000, ambao wameingiliana vyema na Wakenya wengine na huchangia pakubwa uchumi wa nchi), na asilimia 1.6 wanadai hawana uhusiano na dini yoyote ile.
|
20231101.sw_1676_73
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Asilimia 60 ya idadi ya Waislamu huishi katika Mkoa wa Pwani, wakiwa asilimia 50 ya jumla ya wakazi wa pale. Wengi wa wanaoishi sehemu ya magharibi mkoani Pwani ni Wakristo. Eneo la kaskazini la Mkoa wa Mashariki ni makazi ya asilimia 10 ya jumla ya Waislamu nchini; hii ndiyo dini ya wakazi wengi wa hapa, na mbali na idadi ndogo ya Wasomali wanaoishi Nairobi, idadi kubwa ya Wakenya wengine ni Wakristo.
|
20231101.sw_1676_74
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Kenya ni nchi yenye tamaduni anuwai. Tamaduni zinazotambulika ni pamoja na Waswahili walio katika eneo la pwani, jamii za wafugaji katika eneo la kaskazini na jamii nyingine mbalimbali katika maeneo ya kati na magharibi.
|
20231101.sw_1676_75
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Wajaluo wa Kenya ni wazawa wa jamii za wakulima na wafugaji walioishi magharibi mwa Kenya kabla ya ukoloni. Inafahamika kwamba asili ya Wajaluo na makabila mengine ya Waniloti ni kaskazini mwa Kenya, pengine maeneo ya Sudan Kusini ya sasa. Waniloti, kama wanavyoitwa, ni kikundi cha kianthropolojia kilichotoka maeneo ya kaskazini mashariki mwa Afrika. Pengine walihamia kusini kutokana na vita vilivyosababishwa na ukuaji wa Kush na Misri. Waniloti nchini Kenya ni Wajaluo, Waturkana, Wakalenjin na Wamasai. Hili linadhihirika kutokana na kuwepo kwa lahaja zinazofanana kati ya makabila fulani nchini Sudan Kusini leo. Makabila haya ni pamoja na Akoli na Lwo (si sawa na Luo) wanaoishi katika eneo la Darfur.
|
20231101.sw_1676_76
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Kuna makabila mengine ya Waniloti yanayoishi nchini Uganda na Tanzania. Hii hasa ni kwa sababu ya Wajaluo kuvutiwa na Ziwa Victoria, ambako wanapatikana katika nchi hizi tatu (Uganda, Tanzania na Kenya). Nchini Uganda, wanajulikana kwa kuanzisha himaya ya Waganda na ya himaya ya Watoro. Wajaluo nchini Kenya walipigana vita na majirani wao, hasa Wakalenjin, ili kulidhibiti ziwa hilo.
|
20231101.sw_1676_77
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Leo hii, utamaduni wa Wamaasai unajulikana sana kwa kuangaziwa vilivyo na utalii, hata hivyo Wamaasai ni asilimia ndogo ya idadi ya Wakenya kwa jumla. Wamaasai wanatambulika kwa kujipamba sehemu ya juu ya mwili na kwa vito.
|
20231101.sw_1676_78
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Mfumo wa elimu nchini Kenya unajumuisha elimu ya chekechea, ya msingi, ya sekondari na ya vyuo. Elimu ya watoto wadogo aghalabu huchukua miaka mitatu, ya msingi miaka minane, sekondari minne na chuo kikuu miaka minne au sita kwa kutegemea kozi.
|
20231101.sw_1676_79
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Shule za chekechea, ambazo ni za watoto wa umri wa miaka mitatu hadi mitano, ni sehemu muhimu ya mfumo huu wa elimu na ni kigezo muhimu kabla ya kusajiliwa katika darasa la kwanza (Gredi ya Kwanza).
|
20231101.sw_1676_80
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Mwishoni mwa elimu ya msingi wanafunzi hufanya mtihani wa Cheti cha Kuhitimu Masomo ya Msingi Kenya (KCPE), ambao huamua watakaojiunga na shule ya sekondari au vyuo vya ufundi. Umri wa shule ya msingi ni miaka 6/7 hadi 13/14.
|
20231101.sw_1676_81
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Wale wanaojiunga na shule ya upili hufanya mtihani wa taifa mwishoni mwa kidato cha nne - Mtihani wa Cheti cha Kuhitimu Masomo ya Shule ya Upili Kenya (KCSE), ambao huamua watakaojiunga na vyuo vikuu, vyuo vya taatuma nyinginezo au kuajiriwa. Baraza Kuu la Usajili (JAB) ndilo lenye jukumu la kuwachagua wanafunzi watakaojiunga na vyuo vikuu vya umma. Mbali na shule za umma, kuna shule nyingi za binafsi nchini, hasa katika sehemu za miji. Vilevile, kuna shule kadhaa za kimataifa zinazofundisha mifumo mbalimbali ya elimu ya ng'ambo.
|
20231101.sw_1676_82
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Mfumo wa kwanza wa elimu nchini Kenya baada ya uhuru uliletwa na wakoloni Waingereza. Baada ya nchi kupata uhuru tarehe 12 Desemba 1963, Tume ya Ominde iliundwa ili kuleta mabadiliko ambayo yaakisi matarajio ya taifa huru la Kenya. Tume hii ilimulika masuala ya usawa na umoja, ambayo yalikuwa muhimu hasa wakati huo. Mabadiliko ya kilichofundishwa katika historia na jiografia yalifanywa ili kuakisi umoja wa kitaifa. Kati ya miaka 1964 na 1985, mfumo wa 7-4-2-3 ulifuatwa (miaka saba masomo ya msingi, miaka minne sekondari ya daraja la chini, miaka miwili sekondari ya daraja la juu, na miaka mitatu masomo ya chuo kikuu). Shule zote zilifuata mtaala mmoja.
|
20231101.sw_1676_83
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Mwaka wa 1981, kamati iliyoteuliwa na rais kuratibu namna ya kuanzisha chuo kikuu cha pili nchini Kenya, na pia kuubadilisha mfumo wa elimu kwa jumla, ilianza kazi yake. Kamati hii ilipendekeza kuwa mfumo ule wa 7-4-2-3 ubadilishwe kuwa mfumo wa 8-4-4 (miaka minane shule ya msingi, miaka minne shule ya upili, miaka minne elimu ya chuo kikuu). Jedwali lililo katika Elimu ya Sasa Nchini Kenya linaonyesha muundo wa mfumo wa 8-4-4. Ingawa mfumo wa 7-4-2-3 kinadharia ulifikia kikomo mfumo wa 8-4-4 ulipoanzishwa mwaka wa 1985, kundi la mwisho la mfumo huo wa awali lilihitimu kutoka vyuo vikuu vya Kenya mwaka wa 1992.
|
20231101.sw_1676_84
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Mfumo wa sasa wa 8-4-4 ilizinduliwa Januari 1985. Ulitilia mkazo masomo ya kiufundi kwa matarajio kuwa, muundo huu mpya utawawezesha wanaoacha shule katika viwango mbalimbali aidha kujiajiri wenyewe au kupata ajira katika sekta ya juakali.
|
20231101.sw_1676_85
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Mnamo Januari 2003, Serikali ya Kenya ilitangaza kuanzishwa kwa masomo ya shule za msingi bila malipo. Hili lilipelekea kuongezeka kwa wanafunzi waliojiunga na shule za msingi kwa asilimia 70. Hata hivyo, idadi ya waliojiunga na shule za upili na vyuo haikuongezeka sana kwa sababu malipo bado yalihitajika ili kuhudhuria masomo.
|
20231101.sw_1676_86
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Mtihani wa kuhitimu cheti cha masomo ya msingi nchini Kenya (KCPE) hufanywa katika darasa la nane. Matokeo ya mtihani huu huhitajika ili kusajiliwa katika shule ya upili. Mtihani wa kuhitimu cheti cha masomo ya shule ya upili nchini Kenya (K.C.S.E.) hufanywa katika kidato cha nne. Wanafunzi hufanya mtihani katika masomo nane.
|
20231101.sw_1676_87
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Mfumo wa elimu wa Kenya 8-4-4 umepitia mengi magumu katika kipindi kirefu ulichodumu. Punde tu baada ya kufuzu kwa kundi la kwanza la wanafunzi wa mfumo huu mwaka wa 1989, wananchi wengi walijitokeza kuilaumu na kuihukumu serikali kwa kuuanzisha mfumo huu. Wakosoaji hao walidai kuwa waliohitimu hawajaandaliwa vyema na hawangeweza kushindana na wenzao kutoka sehemu nyingine za ulimwengu. Wengine walihoji kuwa waliofuzu kupitia mfumo huu walikuwa aidha wachanga sana au hawajaandaliwa vyema kwa nafasi za kazi zilizokuweko. Serikali haikusikiliza hayo yote pengine kwa sababu uwezekano wa kuubadilisha na kuuunda upya kungeigharimu pesa nyingi.
|
20231101.sw_1676_88
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Hata hivyo, kwa miaka mingi waliofuzu kupitia mfumo huu wamewaaibisha walioupinga kwa kufualu katika vyuo vya nchini na ng’ambo. Pia wasomi na wafanyakazi wa afya kuhamia nchi zilizoendelea ni dhihirisho tosha la hali hii.
|
20231101.sw_1676_89
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Mkazo uliotiliwa masomo ya ufundi umefifia na mabadiliko ya hivi juzi katika mtaala yanasisitiza teknolojia ya upashanaji habari, sayansi, hesabu na lugha. Kwa vyovyote vile, kazi ya kiakademia na kusisitizwa kwa kupita mitihani iliyoandikwa hakujaacha nafasi kwa useremala, uashi, upishi na mafunzo mengine ya ufundi.
|
20231101.sw_1676_90
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Lakini nchi hii inajulikana hasa kwa kutawala katika mbio za masafa ya kadiri na mbio za masafa marefu. Kenya, kwa muda mrefu, imetoa mabingwa wa Olimpiki na michezo ya Jumuia ya Madola katika nyanja mbalimbali, hasa katika mbio za mita 800, mita 1,500, mita 3,000 kuruka viunzi na maji, mita 5,000, mita 10,000 na mbio za masafa marefu. Wanariadha wa Kenya (hasa wa kabila la Wakalenjin) wanaendelea kutawala mbio za masafa ulimwenguni, ingawa ushindani kutoka nchi ya Moroko na Ethiopia umepunguza umaarufu huu.
|
20231101.sw_1676_91
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Wanariadha wa Kenya wanaosifika sana ni pamoja na mshindi mara nne wa mbio za masafa marefu za Boston kwa wanawake na mshindi mara mbili wa mbio za dunia Catherine Ndereba, aliyeshikilia rekodi ya awali ya mbio za dunia Paul Tergat, na John Ngugi.
|
20231101.sw_1676_92
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Wakati wa michezo ya Olimpiki ya Beijing Kenya ilishinda medali 6 za dhahabu, 4 za fedha, 4 za shaba na kulifanya taifa lililofaulu sana barani Afrika katika michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008. Wanariadha wapya walitambulikana, kama Pamela Jelimo, mshindi wa medali ya dhahabu katika mbio za mita 800 kwa wanawake aliyejitahidi na kushinda tuzo la Golden League, na Samuel Wajiru aliyeshinda mbio za masafa marefu kwa wanaume.
|
20231101.sw_1676_93
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Bingwa mstaafu wa mbio za Olimpiki na za Jumuia ya Madola, Kipchoge Keino, alisaidia kuanza ubingwa wa mbio za masafa marefu miaka ya 1970 akafuatwa na bingwa wa michezo ya Jumuia ya Madola, Henry Rono, aliyeshikilia rekodi kadhaa za dunia.
|
20231101.sw_1676_94
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Hivi majuzi, kumekuwa na mzozo wa wanariadha wa Kenya waliosaliti nchi yao na kuwakilisha nchi nyingine, hasa Bahrain na Qatar. Wizara ya michezo ya Kenya imejaribu kuzuia usaliti huu, lakini umeendelea tu, Bernard Lagat akiwa wa mwisho, akichagua kuiwakilisha Marekani. Usaliti huu, kwingi unatokana na sababu za kiuchumi au kifedha ingawa pia wanariadha wazuri wasioweza kufaulu katika timu nzuri ya taifa huona ni rahisi kufaulu kwa kukimbilia nchi nyingine.
|
20231101.sw_1676_95
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Kenya pia imetawala voliboli ya wanawake barani Afrika, huku vilabu na timu ya taifa vikishinda mashindano kadhaa barani Afrika katika mwongo uliopita. Timu ya wanawake pia imeshiriki katika michezo ya Olimpiki na Mashindano ya Ulimwengu ingawa haijafaulu vilivyo.
|
20231101.sw_1676_96
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Mchezo wa kriketi ni maarufu na pia ni mchezo wa timu ambao umefaulu sana. Kenya imeshiriki katika Kombe la Dunia la Kriketi tangu mwaka 1996. Timu hii ilishinda baadhi ya timu maarufu ulimwenguni na kufikia semifainali katika mchuano wa mwaka 2003. Walishinda ligi ya kriketi ya dunia daraja la 1 iliyofanyika Nairobi kwa mara ya kwanza, kisha wakashiriki katika mchuano wa ulimwengu wa T20. Nahodha wa sasa wa timu ni Collins Obuya.
|
20231101.sw_1676_97
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Kenya imejiundia jina katika muungano wa raga. Mchezo huo ni maarufu nchini hasa kwa sababu ya mchuano wa kila mwaka wa Safari Sevens. Timu ya Kenya ya raga ya wachezaji saba kila upande ilikuwa nambari ya 9 katika michezo ya dunia ya wachezaji saba IRB katika msimu wa mwaka 2006.
|
20231101.sw_1676_98
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Kenya ilikuwa bingwa wa soka katika eneo hili lakini ubingwa huu umefifia kutokana na kutoelewana kwa maafisa wa Kamati ya Soka Nchini. Mizozo hii ilipelekea Kenya kupigwa marufuku na FIFA, lakini marufuku hii iliondolewa mnamo Machi 2007.
|
20231101.sw_1676_99
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Kwa upande wa mbio za magari, Kenya ndio waandalizi wa mbio za magari maarufu za Safari Rally zinazotambulika kuwa ngumu zaidi ulimwenguni, na ambazo ni sehemu ya Bingwa wa Mbio za Magari kwa miaka mingi hadi kuondolewa kwake baada ya mbio za 2002 kwa sababu ya matatizo ya kifedha. Baadhi ya madereva maarufu wa mbio za magari ulimwenguni walioshiriki na kushinda mbio hizi ni Bjorn Waldegard, Hannu Mokkola, Tommi Makinen, Shekhar Mehta, Carlos Sainz na Colin McRae. Ingawa mbio hizi bado huendelea kila mwaka kama sehemu ya kutafuta Bingwa wa Mbio za Magari Afrika, waandalizi wanatarajia kuruhusiwa kujiunga tena na Ubingwa wa Magari Ulimwenguni katika miaka michache ijayo.
|
20231101.sw_1676_100
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Ngugi wa Thiong'o ni mmoja wa waandishi maarufu wa Kenya. Kitabu chake :en:Weep Not, Child ni ufafanuzi wa maisha yalivyokuwa Waingereza walipoitwaa Kenya. Hii ni hadithi kuhusu athari za Mau Mau katika maisha ya Wakenya asili. Kinavyochanganya maudhui - ukoloni, elimu, na mapenzi - kunakifanya kuwa kimojawapo kati ya vitabu bora vya hadithi barani Afrika.
|
20231101.sw_1676_101
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Kitabu cha hadithi cha M. G. Vassanji The In-Between World of Vikram Lall kilishinda tuzo la Giller Prize mwaka 2003. Hii ni hadithi ya kubuni ya Mkenya mwenye asili ya Kihindi na familia yake wavyojizatiti na mabadiliko ya kisiasa wakati wa ukoloni na baada ya ukoloni nchini Kenya.
|
20231101.sw_1676_102
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Baada ya uhuru, Kenya iliendeleza ukuaji wa kiuchumi haraka kupitia kwa uwekezaji wa umma, kuhimiza uzalishaji wa kilimo, na kushawishi uwekezaji wa watu binafsi na wageni katika viwanda. Pato la taifa lilikua kwa asilimia 6.6 kuanzia 1963 hadi 1973. Uzalishaji wa kilimo ulikua kwa asilimia 4.7 kila mwaka kwa kipindi hicho ukiwa umechochewa na ugawaji upya wa mashamba, kuanzishwa kwa kilimo cha mimea iliyoimarishwa, na kuanzisha mashamba mapya.
|
20231101.sw_1676_103
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Hata hivyo, kati ya 1974 na 1993 ukuaji wa uchumi wa Kenya ulipungua. Kupungua kwa kilimo kulisababishwa na sera za kilimo zisizofaa, mikopo isiyotosha na vikwazo visiyofaa vya biashara ya kimataifa.
|
20231101.sw_1676_104
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Mnamo mwaka wa 1993, Serikali ya Kenya ilianzisha mpango mkuu wa kuimarisha uchumi na kuufanya huru. Waziri mpya wa fedha na gavana mpya wa Benki Kuu ya Kenya walianza mikakati iliyofuatana kuimarisha uchumi kwa usaidizi wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa). Kama sehemu ya mpango huu, serikali iliondoa usimamizi wa bei za bidhaa, leseni za uagizaji na uthibiti wa ubadilishaji fedha, kubinafsisha kampuni nyingi zilizomilikiwa na umma, kupunguza idadi ya wafanyi kazi wa serikali na kuanzisha sera madhubuti za kulinda fedha. Kuanzia mwaka wa 1994 hadi 1996 ukuaji halisi wa uchumi wa Kenya ulikadiriwa juu kidogo ya asilimia 4 kwa mwaka.
|
20231101.sw_1676_105
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Hata hivyo, kati ya 1997 na 2000, uchumi uliingia kipindi cha kupungua au kutoimarika, kwa sababu ya hali mbaya ya anga na kupungua kwa shughuli za kiuchumi. Mwaka wa 2001 pato la taifa liliimarika kiasi kwani mvua ilirejea kunyesha karibu na viwango vya awali. Ukuaji wa kiuchumi uliendelea kuimarika kiasi mwaka wa 2002 na kufikia asilimia 1.4 mwaka wa 2003, asilimia 4.3 mwaka wa 2004, kisha asilimia 5.8 mwaka wa 2005.
|
20231101.sw_1676_106
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Mnamo Julai 1997, Serikali ya Kenya ilikataa kutimiza makubaliano ya awali na IMF kuhusu mabadiliko ya utawala wake. Jambo hili lilisababisha kukatizwa kwa misaada kwa miaka 3, nayo Benki ya Dunia ikaubana mkopo wa dola milioni 90 za mpango wa kuufufua uchumi. Ingawa mabadiliko mengi ya kiuchumi yaliyofanywa kati ya 1993-94 yalibakia, wataalamu wa maswala ya kiuchumi wasiopendelea mabadiliko waliamini kuwa Kenya iliitaji mabadiliko zaidi, hasa ya kiutawala ili kuongeza ukuaji wa pato la taifa (GDP).
|
20231101.sw_1676_107
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Serikali ya Kenya ilichukua hatua yakini za mabadiliko, pamoja na kuunda Tume ya Kupambana na Ufisadi (KACA), kuanzisha hatua za kuimarisha uwazi wa katika mikakati ya serikali kupata bidhaa na kupunguza fedha inayotumiwa na serikali kulipia mishahara. Mnamo Julai 2000, shirika la IMF lilitia saini dola milioni 150 za Poverty Reduction and Growth Facility (PRGF), nayo Benki ya Dunia ilifuatia na mkopo wa dola milioni 157 kuimarisha uchumi na kuibadilisha sekta ya umma. Mwezi wa Desemba 2000, iliamuliwa kuwa tume ya kupambana na ufisadi haikuwa ya kikatiba na sehemu za juhudi za mabadiliko kukatizwa mwaka 2001. Shirika la IMF na Benki ya Dunia zilikatiza mipango yao. Juhudi zilizofanywa kuanzisha upya mipango hii katikati ya mwaka wa 2002 hazikufaulu.
|
20231101.sw_1676_108
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Chini ya uongozi wa Rais Kibaki, aliyechukua hatamu za uongozi tarehe 30 mwezi wa Desemba 2002, serikali ya Kenya ilianzisha mipango mipya na kabambe ya uimarishaji uchumi na imerejelea ushirikiano wake na Benki ya Dunia na IMF. Serikali mpya ya National Rainbow Coalition (NARC) iliidhinisha Sheria dhidi ya Ufisadi na Uhalifu wa Kiuchumi pamoja na Sheria ya Maadili ya Watumishi wa Umma mnamo Mei 2003 iliyolenga kupiga vita ufisadi katika ofisi za umma. Mabadiliko mengine, hasa katika idara ya sheria, kuagiza bidhaa za umma na kadhalika yamepelekea kurejelewa kwa misaada na matumaini ya kuimarisha uchumi. Kufuatia kupitishwa kwa sheria muhimu za kupambana na ufisadi na serikali mpya, wafadhili walirejelea ufadhili mwezi wa Novemba 2003 na IMF ikaidhinisha msaada wa miaka mitatu wa dola milion 250 ili kupunguza umaskini na kuimarisha uchumi. Wafadhili wakatoa dola bilioni 4.2 kama msaada wa miaka minnne. Kurejelewa kwa ufadhili na kujihusizisha upya kwao kumevutia imani ya wawekezaji.
|
20231101.sw_1676_109
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Mswada wa ubinafsishaji umeidhinishwa ingawa kuanzishwa kwa tume ya ubinafsishaji hakujakamilika, mabadiliko katika utendakazi wa umma yametekelezwa na mwaka wa 2007 Kenya ilishinda tuzo la Umoja wa Kimataifa la Utendakazi wa Umma. Hata hivyo, kazi nyingi zinahitajika kufanywa ili kuiwezesha nchi hii kuyafikia mataifa yaliyoendelea sana kiuchumi, hasa yale ya Mashariki ya Mbali. Changamoto kuu ni pamoja na kuchukua hatua thabiti dhidi ya ufisadi, kupitisha sheria zinazoshughulikia ugaidi na biashara haramu, kutatua upungufu wa ufadhili wa bajeti kisha kurekebisha na kuunda miundo msingi. Inaaminika haya yatasaidia kudumisha sera za kimsingi za kiuchumi, na kuhakikisha ukuaji wa kasi wa kiuchumi uliofikia asilimia 7.2 mwaka wa 2007.
|
20231101.sw_1676_110
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Mwaka wa 2007, serikali ya Kenya ilizindua Ruwaza 2030, ambao ni mpango wa kiuchumi wenye matumaini makuu na ambao ikiwa utatekelezwa kikamilifu, una uwezo wa kuifanya nchi hii kuwa katika kiwango sawa na mataifa yaliyoendelea kiuchumi ya Asia.
|
20231101.sw_1676_111
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Nairobi inaendelea kuwa kituo muhimu na cha kimsingi kwa mawasiliano na biashara cha Afrika Mashariki. Kinajivuna kuwa na miundo msingi ya uchukuzi na mawasiliano bora zaidi katika eneo hili, na wafanyi kazi wenye ujuzi. Makampuni mengi ya kigeni hudumisha matawi yao katika eneo hili ama ofisi za kuyawakilisha mjini Nairobi. Mnamo Machi 1996, Marais wa Kenya, Tanzania na Uganda waliifufua Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC). Shabaha za EAC ni pamoja na kusawazisha kodi na ada zinazotozwa bidhaa, utembeaji huru wa watu na kuimarisha miundo msingi katika eneo hili. Nchi hizi tatu za Afrika Mashariki zilitia saini mkataba wa Customs Union Agreement mwezi wa Machi 2004.
|
20231101.sw_1676_112
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Mwanzoni mwa mwaka wa 2006 Rais wa Uchina, Hu Jintao, alitia saini kandarasi ya utafutaji wa mafuta na Kenya. Haya ndiyo makubaliano ya hivi punde kati ya mfululizo wa mapatano yaliyopagwa kuelekeza maliasili ya Afrika huko Uchina ambako uchumi wake waendelea kukua kwa haraka.
|
20231101.sw_1676_113
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Kandarasi hii iliwezesha kampuni inayoongozwa na taifa la Uchina “offshore oil and gas company” CNOOC Ltd kutafuta mafuta Kenya, ambayo ilianza kuchimba visima vya kwanza mpakani mwa Sudan na Somalia na katika maji ya upwa wake.
|
20231101.sw_1676_114
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kenya
|
Kenya
|
Kenya Coast bibliography. Academic bibliography, hasa kwa Kiingereza, compiled by Jan Hoorweg, Afrika-Studiecentrum, Leiden.
|
20231101.sw_1677_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mombasa
|
Mombasa
|
Mombasa ni mji mkubwa wa pili wa Kenya na wenye bandari muhimu zaidi Afrika Mashariki. Mji huu uko kwenye mwambao wa Bahari Hindi.
|
20231101.sw_1677_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mombasa
|
Mombasa
|
Mombasa ni kitovu cha utalii wa pwani ya Kenya. Watalii wengi hufika kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Moi. Wengine pia husafiri kupitia barabara kutoka Nairobi wakitazama mandhari mbalimbali. Kutoka Nairobi kwenda Mombasa ni takribani kilomita 483.77. Watalii wengi hupenda kuuona mji wa Mombasa kwanza, kisha wanaunganisha ndege hadi Kilimanjaro na sehemu nyingine zilizo na vivutio nchini Tanzania.
|
20231101.sw_1677_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mombasa
|
Mombasa
|
Mnamo mwaka wa 2016, mji wa Mombasa ulikuwa na idadi ya wakazi takriban milioni moja nukta mbili kwenye kisiwa cha Mombasa pamoja na sehemu zake barani. Wengi wao ni Waislamu.
|
20231101.sw_1679_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Togo
|
Togo
|
Togo ni nchi ya Afrika ya Magharibi inayofikia kwenye mwambao wa Ghuba ya Guinea (bahari ya Atlantiki) ikipakana na Benin upande wa mashariki, Burkina Faso kaskazini na Ghana mashariki.
|
20231101.sw_1679_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Togo
|
Togo
|
Togo ni nchi ndogo katika Afrika yenye km² 56,785 pekee kwa umbo la pembenne lenye urefu wa urefu wa kilometa za mraba km 550 na upana wa takriban km 130. Mwelekeo wa eneo la nchi ni kaskazini - kusini.
|
20231101.sw_1679_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Togo
|
Togo
|
Humo kuna kanda zote za kijiografia za Afrika ya Magharibi kuanzia pwani yenye mchanga na misitu ya minazi kusini, vilima vya nyanda za juu katikati na savana pamoja na maeneo yabisi zaidi ya Sahel kaskazini.
|
20231101.sw_1679_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Togo
|
Togo
|
Nchi ilianzishwa kama koloni la Togo ya Kijerumani katika pengo kati ya maeneo ya Uingereza na Ufaransa.
|
20231101.sw_1679_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Togo
|
Togo
|
Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia koloni la Kijerumani liligawiwa kati ya majirani hao kama eneo lindwa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa na baadaye ya Umoja wa Mataifa.
|
20231101.sw_1679_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Togo
|
Togo
|
Mnamo Desemba 1956 wakazi wa Togo ya Kiingereza waliamua kwa kura kubaki na Ghana. Hivyo ni Togo ya Kifaransa pekee iliyopata uhuru mwaka 1960.
|
20231101.sw_1679_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Togo
|
Togo
|
Upande wa dini, mwaka 2020 ilikadiriwa kuwa 47.8% ni Wakristo (hasa wa Kanisa Katoliki) 33% wanafuata dini asilia za Kiafrika na 18.4% ni Waislamu (hasa Wasuni).
|
20231101.sw_1679_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Togo
|
Togo
|
Mwakikagile, Godfrey, Military Coups in West Africa Since The Sixties (Nova Science Publishers, Inc., 2001).
|
20231101.sw_1679_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Togo
|
Togo
|
Piot, Charles, Nostalgia for the Future: West Africa After the Cold War (University of Chicago Press, 2010).
|
20231101.sw_1679_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Togo
|
Togo
|
Schnee, Dr. Heinrich, German Colonization, Past and Future – the Truth about the German Colonies (George Allen & Unwin, 1926).
|
20231101.sw_1679_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Togo
|
Togo
|
Sebald, Peter, Togo 1884 bis 1914. Eine Geschichte der deutschen "Musterkolonie" auf der Grundlage amtlicher Quellen (Berlin, 1987).
|
20231101.sw_1679_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Togo
|
Togo
|
Seely, Jennifer, The Legacies of Transition Governments in Africa: The Cases of Benin and Togo (Palgrave Macmillan, 2009).
|
20231101.sw_1679_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Togo
|
Togo
|
Zurstrassen, Bettina, "Ein Stück deutscher Erde schaffen". Koloniale Beamte in Togo 1884–1914 (Frankfurt/M., Campus, 2008) (Campus Forschung, 931).
|
20231101.sw_1686_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani
|
Pangani
|
* Mto wa Pangani unabeba maji ya Milima ya Meru, Kilimanjaro, Pare na Usambara kwenda Bahari Hindi. Mdomo wake uko mjini Pangani.
|
20231101.sw_1686_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani
|
Pangani
|
* Mji wa Pangani ni makao makuu wa wilaya ya Pangani iliyomo mkoa wa Tanga ufukoni mwa Bahari ya Hindi na mto wa Pangani.
|
20231101.sw_1686_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Pangani
|
Pangani
|
Jina la Pangani hupatikana pia katika miji mbalimbali likitaja eneo au mtaa ndani yake, kwa mfano Pangani katika Nairobi, karibu na Eastleigh. Maana ni "eneo watu walipopanga nyumba zao".
|
20231101.sw_1696_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mhanga
|
Mhanga
|
Mhanga (pia muhanga, fundi-mchanga, kiharara, kukukifuku au loma; jina la kisayansi: Orycteropus afer) ni mnyama wa Afrika aliye spishi pekee ya oda Tubulidentata ambayo inaishi hadi sasa.
|
20231101.sw_1701_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Wamasai ni kabila la watu wanaopatikana Kenya na Tanzania. Kwa sababu ya mila zao, mavazi tofauti na kuishi karibu na mbuga nyingi za Afrika Mashariki, ni miongoni mwa makabila yanayojulikana zaidi hata nje ya Afrika.
|
20231101.sw_1701_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Wao wanazungumza Maa, mojawapo ya lugha za familia ya lugha za Kinilo-Sahara inayohusiana na Kidinka na Kinuer. Kwa sababu ya uhamaji, Wamasai ndio wazungumzaji wa Kiniloti wanaoishi kusini zaidi. Pia wameelimika katika lugha rasmi za Kenya na Tanzania: Kiswahili na Kiingereza.
|
20231101.sw_1701_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Utafiti juu ya DNA yao umeonyesha walivyoathiriwa na urithi wa nasaba mbalimbali, hata kutoka nje ya Afrika, lakini hasa wa jamii ya Wakushi wa Afrika Mashariki.
|
20231101.sw_1701_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Idadi ya Wamasai wa Kenya ilihesabiwa kuwa 1,189,522 katika sensa ya mwaka 2019 na wale wa Tanzania walikadiriwa kuwa 800.000 katika mwaka 2011 ; kwa jumla inakadiriwa kuwa 2,000.000 Makadirio hayo ya Wamasai katika nchi zote mbili huenda ikawa vigumu kuyathibitisha kwa sababu ya umbali wa maeneo ya vijiji vyao vingi, na asili yao ya uhamaji.
|
20231101.sw_1701_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Kwa asili walikuwa wafugaji na hivyo walihamahama, na sehemu bado wanaishi maisha ya namna hiyo. Ingawa serikali za Tanzania na Kenya zimeweka mipango kuwahimiza Wamasai kuachana na jadi ya uhamaji ili kuishi maisha ya kisasa, bado wameendelea na desturi hiyo. Wao wanadai haki ya kulisha mifugo katika Hifadhi za Taifa katika nchi zote mbili. Hivi majuzi, Oxfam imedai ni lazima mtindo wa maisha wa Wamasai ukubaliwe kwa kuzingatia mabadiliko ya hali ya hewa kwa sababu hawawezi kulima katika majangwa.
|
20231101.sw_1701_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Kulingana na historia simulizi yao wenyewe, asili ya Wamasai ni kwenye bonde la Nile ya chini, kaskazini kwa Ziwa Turkana (Kenya kaskazini magharibi).
|
20231101.sw_1701_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Walianza kuhamia kusini karibu na karne ya 15, wakiwasili katika shina la ardhi kutoka kaskazini mwa Kenya na Tanzania ya kati tangu karne ya 17 hadi mwisho wa karne ya 18. Makabila mengine yalilazimishwa kuyahama makazi yao Wamasai walipohamia huko.
|
20231101.sw_1701_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Eneo la Wamasai lilifikia kilele cha ukubwa wake katikati ya karne ya 19, na kuenea kote katika Bonde la Ufa na pande za ardhi kutoka Mlima Marsabit huko kaskazini hadi Dodoma huko kusini. Wakati huo Wamasai, na vilevile kundi kubwa la waliokuwa wamejiunga nalo, walikuwa wakivamia mifugo hadi umbali wa mashariki ya pwani ya Tanga huko Tanzania. Washambuliaji walitumia mikuki na ngao, lakini walikuwa wamehofiwa kwa kutupa vilabu (orinka) walivyoweza kutupa kwa usahihi kutoka umbali wa mita 100.
|
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.