_id
stringlengths 15
22
| url
stringlengths 31
150
| title
stringlengths 1
86
| text
stringlengths 100
23.8k
|
---|---|---|---|
20231101.sw_1701_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Mwaka 1852 kulikuwa na ripoti ya msongamano wa wapiganaji 800 wa Kimasai kuhamia nchini Kenya. Mwaka 1857, baada ya kufyeka "Nyika ya Wakuafi" kusini mashariki mwa Kenya, washambuliaji Wamasai wakatisha Mombasa pwani mwa Kenya.
|
20231101.sw_1701_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Kipindi cha upanuzi ulifuatwa na "Emutai" ya miaka 1883-1902. Kipindi hicho kiliainishwa na uenezi wa magonjwa ya bovin pleuropneumonia, tauni ya ng'ombe na ndui. Kisio la kwanza la mwanajeshi wa Kijerumani huko kaskazini magharibi mwa Tanganyika ni kwamba asilimia 90 ya ng'ombe na nusu ya wanyamapori walikufa kutokana na ugonjwa wa tauni. Madaktari Wajerumani walidai kuwa katika eneo moja "kila sekunde" Afrika kulikuwa na mtoto aliyeugua matokeo ya ndui. Kipindi hicho kiliambatana na ukame. Mvua ilikosa kunyesha kabisa miaka 1897 na 1898.
|
20231101.sw_1701_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Mtafiti kutoka Austria, Oscar Baumann akisafiri katika nchi ya Wamasai miaka 1891-1893, alieleza makazi huko katika volkeno ya Ngorongoro katika kitabu cha mwaka 1894 durch Massailand zur Nilquelle ("Kupitia nchi ya Wamasai kwenye chanzo cha Nile"): "Kulikuwa na wanawake waliodhoofiwa mno waliotazama ule wazimu wa njaa ... mashujaa waliokuwa wameshindwa kutembea, wakiwa na wazee walioathirika na wasiojali kitu. Vikundi vya tai viliwafuata kutoka juu, wakisubiri waathirika. " Kulingana na kisio moja theluthi mbili za Wamaasai walikufa katika kipindi hicho.
|
20231101.sw_1701_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Kuanzia mkataba wa mwaka 1904, na kufuatiwa na mwingine wa mwaka 1911, ardhi ya Wamasai nchini Kenya ilipunguzwa kwa asilimia 60 wakati Waingereza walipowafukuza ili kutayarisha mashamba ya wakoloni, na hatimaye kuwalazimu kuishi katika wilaya ya Kajiado na Narok.
|
20231101.sw_1701_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Wamasai wa Tanzania walifukuzwa kutoka ardhi yenye rutuba kati ya Mlima Meru na Mlima Kilimanjaro, nyanda yenye rutuba iliyo karibu na Ngorongoro katika miaka ya 1940. Ardhi zaidi ilichukuliwa kwa ajili ya hifadhi ya wanyamapori na hifadhi za taifa: Amboseli, Nairobi, Masai Mara, Samburu, Ziwa Nakuru, na Tsavo nchini Kenya; Manyara, Ngorongoro, Tarangire na Serengeti huko Tanzania.
|
20231101.sw_1701_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Jamii ya Wamasai haijawahi kukubali kamwe usafirishaji haramu wa binadamu, na wote waliotafuta watumwa walikuwa wakiwaepuka Wamasai. Pamoja na kusimama dhidi ya utumwa, waliishi pamoja na wanyama pori wengi huku wakikataa kula wanyama hao wala ndege. Hivyo sasa ardhi ya Wamasai ina Hifadhi za Wanyamapori zilizo bora kabisa kote Afrika Mashariki.
|
20231101.sw_1701_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Kimsingi kuna jamii kumi na mbili za kabila la Wamasai, kila jamii ikiwa na desturi, muonekano, uongozi na lugha tofauti. Jamii hizo zinajulikana kama Keekonyokie, Daha Besdi, Purko, Wuasinkishu, Siria, Laitayiok, Loitai, Kisonko, Matapato, Dalalekutuk, Loodokolani na Kaputiei.
|
20231101.sw_1701_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Jamii ya Wamasai inafuata sana mfumo dume: katika desturi yao ni wanaume, pamoja na wazee wastaafu, wanaoamua mambo makubwa zaidi kwa kila kikundi cha Wamasai.
|
20231101.sw_1701_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Sheria simulizi zinashughulikia masuala mengi ya desturi. Kunyongwa kisheria hakujulikani, na malipo ya kawaida kwa ng'ombe hutosheleza mambo. Kuna mbinu za kutatua migogoro nje ya mahakama kama 'amitu', inayomaanisha 'kufanya amani', au 'arop', ambayo inahusisha kuomba msamaha wa dhati.
|
20231101.sw_1701_17
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Wamasai humwabudu Mungu pekee, nao humwita Enkai au Engai. Engai ni Mungu mmoja mwenye asili mbili: Engai Narok (Mungu Mweusi) ana huruma, na Engai Nanyokie (Mungu Mwekundu) ana ghadhabu.
|
20231101.sw_1701_18
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
"Mlima wa Mungu", Ol Doinyo Lengai, uko kaskazini mwa Tanzania. Mtu mkuu katika mfumo wa dini ya Wamasai ni laibon ambaye anaweza kushiriki katika: uponyaji wa kidini, kuzungumza na Mungu na unabii, kuhakikisha mafanikio katika vita au mvua ya kutosha. Nguvu zozote alizokuwa nazo laibon zilikuwa zimetokana na utu au nafsi yake, si cheo chake. Kwa sasa Wamasai wengi wamekuwa Wakristo, na kwa kiwango kidogo Waislamu.
|
20231101.sw_1701_19
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Vifo vingi vya watoto wachanga miongoni mwa Wamasai vimesababisha watoto wengi kutotambuliwa mpaka kufikia umri wa miezi 3, ilapaitin. Kwa utamaduni, mwishoni mwa maisha yao Wamasai huzikwa bila sherehe na maiti wanaachwa nje waliwe na tumbusi Maiti kukataliwa na tumbusi na fisi, wanaojulikana kama Ondili ama Oln'gojine, huonekana kuwa kitu kibaya, na kusababisha jamii ya mfu huyo kulaumiwa. Kwa hiyo haikuwa nadra kupaka miili mafuta na damu ya ng'ombe aliyechinjwa. Mazishi ya zamani yalikuwa yametengwa kwa waheshimiwa wakubwa, kwani iliaminika kuwa mazishi yalidhuru udongo.
|
20231101.sw_1701_20
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Maisha ya Wamasai inahusika sana na ng'ombe, ambao huwa msingi wa chakula chao. Kipimo cha mali ya mtu ni idadi ya mifugo na watoto alionao. Kuwa na ng'ombe 50 au zaidi kunaheshimika, na watoto wengi zaidi ni bora. Mtu ambaye anao wengi upande mmoja lakini si upande wa pili anahesabiwa kama maskini.
|
20231101.sw_1701_21
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Wamasai huamini kwamba Mungu aliwapa wao ng'ombe wote duniani, kwa hiyo kuchukua mifugo kutoka makabila mengine ni suala la kudai haki yao, lakini zoezi hili limepungua.
|
20231101.sw_1701_22
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Katika Bonde la Ufa, ambako kabila hilo liliishi kwa karne nyingi, hakukuwa na malaria, hakuna magonjwa ya ng'ombe, hakuna nzi wanaovamia na kusababisha magonjwa kwa mifugo na ugonjwa hatari kwa watu.
|
20231101.sw_1701_23
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Mwanzoni mwa karne iliyopita, wakoloni waliingia Afrika Mashariki. Kabila la Wamasai daima limepinga kwa uthabiti utumwa na kuishi karibu na wanyama wengi wa pori duniani, bila kutaka kula ndege na wanyamapori na ni moja la machache yaliyoweka upinzani mkali kwa wakoloni wa Kiingereza. Kwa takriban miaka kumi (1890-1900), Wamasai walipigania ardhi zao kwa mikuki dhidi ya bunduki za wakoloni. Waliuawa kwa maelfu, na pia ng'ombe, kondoo na mbuzi kuibiwa na kutumika kulisha majeshi yaliyowavamia. Kufikia 1901-1902 kabila la Wamaasai lilishindwa.
|
20231101.sw_1701_24
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Mnamo 1904, Waingereza waliwalazimisha Wamasai waliokatishwa tamaa kuondoka kwenye malisho yenye rutuba ya Bonde la Ufa na kuhamia nchi za kusini (eneo la Mbuga ya Masai Mara ya sasa).
|
20231101.sw_1701_25
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Waingereza walilazimisha kusainiwa kwa makubaliano, ambayo wao wenyewe walighairi miaka saba baadaye kwa sababu walitaka ardhi zaidi kwa makazi ya Wazungu. Mnamo 1911, makubaliano mengine yalitiwa saini, ambayo wavamizi pia hawakuzingatia.
|
20231101.sw_1701_26
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Kihistoria Wamaasai ni watu wanaohamahama, kwa hiyo tangu jadi wamekuwa wakitumia vinavyopatikana kwa urahisi ili kujenga makazi yao. Nyumba zao za asili ziliundwa kwa ajili ya kuhama mara kwa mara, kwa hiyo hazikujengwa za kudumu.
|
20231101.sw_1701_27
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Inkajijik (nyumba hizo) zina umbo la nyota au mviringo, na hujengwa na wanawake. kwa mbao, matawi madogo yaliyochanganywa na matope, vijiti, majani, kinyesi cha ng'ombe, mkojo wa binadamu, na majivu. Mavi ya ng'ombe inahakikisha kuwa paa halivuji, na maji ya mvua yasiweze kupita.
|
20231101.sw_1701_28
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Enkaji ni ndogo, kipimo cha mita 3x5 na kimo cha m 1.5 kwenda juu. Ndani ya nafasi hiyo familia hupika, hula, hulala, hupiga gumzo na huweka akiba ya chakula, mafuta na mali nyingine. Mifugo wadogo mara nyingi pia huwekwa ndani ya enkaji.
|
20231101.sw_1701_29
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Vijiji huzungukwa na ua (Enkang) lililojengwa na wanaume kwa kutumia miiba ya acacia, mti wa asili. Usiku wote ng'ombe, mbuzi na kondoo huwekwa katikati ya ua hilo, kuwalinda kutokana na wanyamapori.
|
20231101.sw_1701_30
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Kitengo kati ya jamii ya Wamasai ni umri. Ingawa wavulana hutumwa nje na ndama na kondoo kuanzia utotoni, utoto kwa wavulana ni wakati wa kucheza, isipokuwa kuchapwa viboko kidesturi ili kuthibitisha ujasiri na uvumilivu. Wasichana huwajibika katika kazi ndogondogo kama vile kupika na kukamua ng'ombe, ujuzi ambao hujifunza kutoka kwa mama zao kuanzia umri mdogo.
|
20231101.sw_1701_31
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Kila baada ya miaka 15 hivi, kizazi kipya cha Morans au Il-murran (wapiganaji) kitatahiriwa. Hii inahusisha wavulana wengi kati ya umri wa miaka 12 na 25, ambao wamebalehe na si wa kizazi kilichopita. Moja ya sherehe ya kupita ujana hadi upiganaji ni sherehe ya tohara, ambayo inafanywa bila dawa ya kugandisha misuli. Hii tohara hufanywa na wazee, ambao hutumia kisu chenye makali na kigozi cha ng'ombe kufunika jeraha. Neno la Kimasai kwa tohara ni 'emorata'. Kijana lazima avumilie operesheni akiwa kimya. Kuonyesha maumivu huleta aibu, angalau kwa muda. Maneno yoyote ya mshangao yanaweza kusababisha makosa katika operesheni hiyo nyeti, ambayo inaweza kuleta matatizo mengi, majeraha zaidi, na maumivu. Mchakato wa uponyaji utachukua miezi 3-4, wakati ambao kuna uchungu kwenda haja ndogo na wakati mwingine hata hauwezekani, na wavulana lazima wabaki katika nguo nyeusi kwa kipindi cha miezi 4-8.
|
20231101.sw_1701_32
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Katika kipindi hicho, wavulana waliotahiriwa wataishi katika "manyatta", yaani "kijiji" kilichojengwa na mama zao. Manyatta hizo hazina nyua za kulinda boma, ili kusisitiza jukumu lao la kulinda jamii. Hakuna ua la mifugo linalojengwa, kwa sababu wapiganaji hawana ng'ombe wala hawana jukumu la kufuga.
|
20231101.sw_1701_33
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Ibada za kifungu zaidi zinahitajika kabla ya kufikia hadhi ya mpiganaji mwandamizi, ikifikia upeo katika sherehe ya 'eunoto', yaani "ujio wa umri".
|
20231101.sw_1701_34
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Wakati kizazi kipya cha mashujaa kinaanzishwa, waliokuwa ilmoran huendelea kuwa "wazee bila mamlaka", ambao huwajibika kwa maamuzi ya kisiasa hadi wafanywe "wazee wenye mamlaka".
|
20231101.sw_1701_35
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Wapiganaji wana jukumu la usalama katika jamii, na hutumia muda wao mwingi wakizuru ardhi yao, pia hupita mipaka yao. Pia wanazidi kushiriki katika biashara ya mifugo kuliko awali, kuendeleza na kuboresha hisa za msingi kupitia biashara na kubadilisha bidhaa.
|
20231101.sw_1701_36
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Wavulana wana wajibu wa kuwalinda mifugo wadogo. Katika msimu wa ukame, wote wapiganaji kwa wavulana huchukua jukumu la ufugaji. Wazee ni wakurugenzi na washauri wa shughuli za kila siku. Wanawake wana jukumu la ujenzi wa nyumba, na vilevile kuchota maji, kuokota kuni, kukamua ng'ombe na kupikia familia.
|
20231101.sw_1701_37
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Hadithi moja kuhusu Wamasai ni kwamba kila kijana anatakiwa kuua simba kabla atahiriwe. Ingawa simba walikuwa wanawindwa zamani, na uwindaji huo umepigwa marufuku katika Afrika Mashariki, bado simba huwindwa wanapowaua mifugo, na vijana mashujaa wanaohusika katika mauaji hayo hupewa heshima kuu. Kutokana na wasiwasi kuhusu idadi ya simba nchini, kuna mpango wa kulipa fidia wakati simba anapowua mifugo, badala ya uwindaji na kuua simba. Hata hivyo, kuua simba mmoja kuna thamani kubwa na heshima katika jamii.
|
20231101.sw_1701_38
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Wasichana pia hutahiriwa ('emorata') wanapobalehe na hupewa maelekezo na ushauri zinazohusiana na majukumu yao mapya, wanasemekana kuwa wamehitimu umri wa wanawake, tayari kuolewa. Ukeketaji nchini Kenya unatekelezwa kwa 38% ya wakazi. Namna ya kawaida ni clitorectomy. Tendo hilo linaweza kusababisha kovu nene ngozini, ambalo linafanya vigumu kwenda haja ndogo, na hii pia umeleta utata. Ukeketaji ni haramu nchini Kenya na Tanzania na huleta ukosoaji mwingi kutoka nje ya nchi zote mbili na hata kutoka kwa wanawake ambao wameupitia, kama vile Mmasai mwanaharakati Agnes Pareiyo. Ni hivi majuzi katika sehemu mbalimbali imebadilishwa na "kukatwa kwa maneno", sherehe kuwashirikisha kuimba na kucheza katika nafasi ya ukeketaji. Hata hivyo, unabakia na thamani kwa utamaduni. Baadhi wanafikiria ni muhimu kwa sababu Wamasai wanaume wanaweza wakakataa mwanamke asiyetahiriwa, eti haoleweki, au sivyo mahari yake itapunguzwa.
|
20231101.sw_1701_39
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Tohara hizo ni kawaida kufanywa na 'mtekelezaji' ambaye mara nyingi si Mmasai, kwa kawaida hutoka kwa Wandorobo. Visu vya tohara hutengenezwa na wafua-chuma, 'il-kunono', ambao huepukwa na Wamaasai kwa sababu ya kutengeneza silaha za kifo (visu, panga fupi ('ol alem'), mikuki, n.k.). Sawa na wanaume vijana, wanawake ambao wamekeketewa huvaa nguo nyeusi, hujipaka rangi na alama kwenye nyuso, na kisha kufunika nyuso zao wanapokamilisha sherehe.
|
20231101.sw_1701_40
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Wanawake walioolewa wanapokuwa waja wazito huruhusiwa kutofanya kazi nzito kama kukamua ng'ombe na kuokota kuni. Mahusiano ya kingono pia yanapigwa marufuku.
|
20231101.sw_1701_41
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Wamasai huoa wake wengi; hii hutendwa ili kukabiliana na vifo vingi vya watoto wachanga na wapiganaji. Kuolewa na wanaume wengi pia kunakubaliwa: mwanamke huolewa si na mumewe tu, lakini umri mzima wa kikundi chake. Wanaume hutarajiwa kumpa mgeni wa rika lake kitanda na mwanamke. Mwanamke anaamua mwenyewe kama atajiunga na mtu huyo. Mtoto yeyote atakayezaliwa ni mtoto wa mume katika utaratibu wa Kimasai.
|
20231101.sw_1701_42
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
"Kitala", aina ya talaka au kukimbilia, inawezekana katika nyumba ya mke wa baba, kwa sababu ya kumdhulumu mke. Kurudisha mahari, ulinzi wa watoto, n.k. hukubaliwa baadaye.
|
20231101.sw_1701_43
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Wamasai ni watu wa jadi na hawabadili utamaduni wao kwa vikubwa. Hata hivyo, hii inabadilika polepole. Wamasai wanaanza kuvaa mavazi za kisasa pia.
|
20231101.sw_1701_44
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Desturi moja ambayo inabadilika ni arusi. Wasichana wanaolewa wakati wapo kati ya umri wa miaka kumi na mbili na ishirini. Lakini, mila hii inabadilika kwa sababu wasichana wanaenda elimu ya juu na hawawezi kuanza famila bado.
|
20231101.sw_1701_45
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Siku kabla ya harusi, mume ataleta mwisho wa mahari iliyokubaliwa kwa familia ya msichana. Mahari kwa kawaida ni fedha, ng’ombe, mablanketi, na asali pamoja. Siku hiyo, msichana ananyolewa kichwa chake kama ishara ya mwanzo wake mpya. Hata hivyo, wanawake wa Kimasai wengi hawana nywele na wanaweka kichwa chao. Harusi inaanza na baraka kutoka kwa mzee. Yeye hutoa maziwa karibu na nyumba ya mama wa msichana. Kabla ya msichana kuondoka nyumbani, amefungwa nyasi katika viatu vyake. Hii ni baraka pia kwa sababu nyasi inaashiria wingi kwa Maasai watu.
|
20231101.sw_1701_46
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Watu kutoka kijiji cha msichana wanamtembelea kabla ya kuondoka na wanaahidi zawadi. Msichana hufunga fimbo katika mkufu wake kwa kila zawadi.
|
20231101.sw_1701_47
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Inaitwa enkariwa na hii inamkumbusha ngapi anavyopaswa kukusanya baada ya harusi. Kisha, sherehe iko katika kijiji cha mtu huyo. Wakati bibi inapofika, yeye anapokea mtoto kuwaonyesha watoto ambao atakuwa nao. Kukabili mashariki, ishara ya mwanzo mpya, wanaarusi hupata baraka za Kimasai kutoka kwa mzee wa Kimasai kutoka kwa jamii. Kisha, wanakula mbuzi na wanacheza muziki.
|
20231101.sw_1701_48
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Muziki wa kitamaduni wa Kimasai huwa na sauti kutoka kwaya ya waimbaji huku kiongozi wa nyimbo, 'Olaranyani', huimba kiitikio. Olaranyani kwa kawaida ni yule mwimbaji bora ambaye anaweza kuimba wimbo huo, ingawa watu kadhaa huweza kuongoza wimbo. Olaranyani huanza kwa kuimba mstari kichwa (namba) cha wimbo. Kikundi basi kitajibu kwa kukubali, na Olaranyani ataimba mistari huku kikundi kikiimba. Kila wimbo una namba maalum kulingana na kuita-na-kuitika. Mipangilio ya nyimbo ya kawaida huwa ya 5 / 4, 6 / 4 na 3 / 4 wakati saini. Maneno hufuata maudhui maalumu na hurudiwa mara nyingi baada ya muda. Kutingisha shingo huongozana na kuimba. Wakati wa kupumua kichwa huelekezwa mbele. Kichwa huelekezwa nyuma kwa ajili ya kuvuta pumzi. Kwa ujumla hii hueneza ratiba ya sauti zao.
|
20231101.sw_1701_49
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Wanawake huimba nyimbo tulivu, na nyimbo za kuwasifu watoto wao. Namba, ule mfano wa wito-na-majibu, marudio ya misemo isiyokuwa na maana, misemo ifuatayo kila mstari kwa kurudiwarudiwa, na waimbaji kukabiliana na mistari yao ni ishara ya kuimba kwa wanawake. Wakati wanawake wamasai wengi hukusanyika pamoja, wao huimba na kucheza kati yao wenyewe.
|
20231101.sw_1701_50
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Wamasai hutumia sauti zao pekee wanapoimba, isipokuwa wanapotumia pembe la Greater Kudu kuwaalika Wamoran kwa sherehe ya Eunoto
|
20231101.sw_1701_51
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Kuimba na kucheza wakati mwingine hufanyika katika manyatta, na kuhusisha kutaniana. Wavulana hupiga foleni na kuimba, "Oooooh-yah", kwa kikohozi, pamoja na msukumo wa miili yao. Wasichana husimama mbele ya wanaume na kusokota miili huku wakiimba "Oiiiyo .. yo" katika kuwajibu wanaume. Ingawa miili yao hukaribiana, hawagusani.
|
20231101.sw_1701_52
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Eunoto, sherehe ya kubalehe kwa mpiganaji, inaweza kuhusisha siku kumi au zaidi za kuimba, kucheza na ibada. Wapiganaji wa Il-Oodokilani hufanya aina ya mchezo inayoitwa adumu, au aigus, mara nyingine inajulikana kama "ngoma ya kuruka". (adumu na aigus ni vitenzi vinavyomaanisha "kuruka" na adumu humaanisha "Kuruka juu na chini katika ngoma" Wapiganaji hujulikana vizuri, na mara nyingi hupigwa picha, katika ushindani huo wa kuruka. Wapiganaji huingia katika mviringo, na moja au wawili wataingia kati ya mviringo kuanza kuruka, bila kuacha visigino vyao kugusa ardhi. Wajumbe wa kikundi wanaweza kuongeza sauti zao kwa kuzingatia urefu wa wanavyoruka.
|
20231101.sw_1701_53
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Washikaji wa Moran ('intoyie') hujitembeza katika nguo maridadi kuvutia wengi wao kama mmojawapo ya eunoto. Mama wa Moran huimba na kucheza kuonyesha heshima kwa ujasiri wa watoto wao.
|
20231101.sw_1701_54
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Wanamuziki wa Hip Hop wa kisasa, X Plastaz, kutoka kaskazini mwa Tanzania wamechanganya sauti na midundo ya Wamasai katika muziki wao.
|
20231101.sw_1701_55
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Kutoboa na kunyosha ndewe ni kawaida ya Wamasai. Vifaa mbalimbali hutumika kutoboa na kunyosha masikio, kama vile miiba kwa kutoboa, ukuti, mawe, msalaba, sehemu ya jino la tembo n.k. Idadi ya Wamasai wanaofuata desturi hiyo, hasa wavulana, inazidi kupungua.
|
20231101.sw_1701_56
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Kung'oa jino mojawapo kati ya machonge mapema utotoni ni zoezi ambalo limetiwa kumbukumbu katika Wamasai wa Kenya na Tanzania. Kuna imani kati ya Wamasai kuwa kuhara, kutapika na magonjwa mengine yanayoathiri watoto husababishwa na kuvimba kwa mizizi ya meno, ambayo hufikiriwa kuwa na 'minyoo' au ni 'meno ya karatasi' au 'meno ya plastiki'. Imani hiyo si ya pekee kwa Wamasai. Vijijini Kenya katika kundi la watoto 95 wenye umri kati ya miezi sita na miaka miwili waliotahiniwa mwaka 1991/92, 87% walipatikana kuwa wameng'olewa jino moja au zaidi. Katika kundi la watoto wa umri wa miaka 3-7, 72% ya watoto walikuwa hawana meno ya kusiaga.
|
20231101.sw_1701_57
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Kijadi, Wamasai hula nyama, maziwa na damu ya ng'ombe. Utafiti wa ILCA (Nestel 1989) unasema: "Leo hii, chakula kikuu cha Kimasai ni maziwa ya ng'ombe na unga wa mahindi. Wao huyanywa maziwa pekee au katika chai na unga wa mahindi hutumiwa kupika uji au ugali. Unga ulioshikamana unajulikana kama ugali na huliwa na maziwa; na hii inatofautiana na uji, ambayo hutayarishwa na hupikwa na maziwa. Nyama, ingawa ni chakula muhimu, huliwa kwa nadra, kwa hiyo haiwezi kutambulika kama chakula kikuu. Mafuta ya nyama hutumika katika kupika, sanasana uji, mahindi na maharagwe. Siagi pia ni chakula muhimu cha watoto wachanga. Damu hunywewa kwa nadra."
|
20231101.sw_1701_58
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Utafiti wa International Livestock Centre for Africa (Bekure et al. 1991) unaonyesha mabadiliko makubwa sana katika mlo wa Kimasai kuelekea bidhaa zisizo za mifugo pamoja na mahindi kuwa asilimia 12-39 na sukari asilimia 8-13; na wastani wa lita moja ya maziwa hunywewa na kila mtu kwa siku.
|
20231101.sw_1701_59
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Maziwa hayo hutumika sanasana kama maziwa lala au maziwa-siagi - maziwa yaliyochanganywa na siagi. Maziwa hutumika sana. Mahitaji ya protini huwa yametoshelezwa kikamilifu. Hata hivyo, ugavi wa chuma, niasini, vitamini C, vitamini A, thiamine na nguvu haviwezi kupatikana kikamilifu kwa kunywa maziwa pekee. Kutokana na kubadilika kwa mazingira, hasa msimu wa ukame wa mara kwa mara, wafugaji wengi, pamoja na Wamasai, hutumia nafaka katika maakuli .
|
20231101.sw_1701_60
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Wamasai hufuga ng'ombe, mbuzi na kondoo, pamoja na kondoo mwekundu, vilevile ng'ombe waliothaminiwa zaidi. Vipimo vya moyo vilitumiwa kwa wavulana Wamasai 400 na hakukuwa na ushahidi wowote wa ugonjwa wa moyo, upungufu au ulemavu. Utafiti zaidi ulionyesha kuwa wastani wa kiwango cha mafuta moyoni ulikuwa asilimia 50 za wastani wa Wamarekani. Matokeo hayo yalithibitisha afya ya Wamoran, ambayo ilitathminiwa kama "kiwango cha Olimpiki".
|
20231101.sw_1701_61
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Supu pengine ni mmojawapo ya matumizi muhimu zaidi ya mimea kwa chakula cha Wamasai. Acacia nilotica ni mmea wa supu unaotumika mara nyingi. Mzizi au shina huchemshwa katika maji na kutumiwa peke yake au huongezwa kwa supu. Wamasai hupenda kuichukua kama dawa, na inajulikana kuwafanya jasiri, wenye nguvu na washindani. Wamasai hunywa supu yenye gome na mizizi inayopunguza mafuta moyoni; Wamasai wanaoishi mijini, ambao hawana mimea hiyo, hupatwa na maradhi ya moyo.
|
20231101.sw_1701_62
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Ingawa yanatumiwa kama vitafunio, matunda huwa sehemu kubwa ya chakula cha watoto na wanawake wanaochunga wanyama na pia moran jangwani.
|
20231101.sw_1701_63
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Kuchanganya damu ya ng'ombe na maziwa inafanywa kuandaa kinywaji cha kitamaduni katika sherehe za pekee na pia kama chakula kwa wagonjwa. Hata hivyo, kuchanganya damu katika mlo unadidimia kutokana na kupunguka kwa idadi ya mifugo.
|
20231101.sw_1701_64
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Hivi majuzi, Wamasai wamekuwa wakitegemea vyakula kutoka maeneo mengine kama vile unga wa mahindi, mchele, viazi, kabichi (zinazojulikana na Wamasai kama majani ya mbuzi) n.k. Wamasai ambao wanaishi karibu na wakulima wameshughulikia kilimo kama msingi wa kujikimu. Katika maeneo hayo, mashamba hayo hayawezi kudumisha idadi kubwa ya wanyama; hivyo Wamaasai hulazimika kulima.
|
20231101.sw_1701_65
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Mavazi hutofautiana kadiri ya umri, jinsia, na mahali. Vijana wa kiume, kwa mfano, huvaa nguo nyeusi kwa miezi kadhaa inayofuata tohara. Hata hivyo, nyekundu ni rangi iliyopendelewa. Bluu, nyeusi na milia huvaliwa kama zilivyo miundo na rangi za Kiafrika.
|
20231101.sw_1701_66
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Wamasai walianza kubadilisha ngozi ya wanyama, ndama na kondoo ili kutumia nguo za pamba katika miaka ya 1960.
|
20231101.sw_1701_67
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Mashuka ni vitambaa vinavyozungushwa mwilini, juu ya kila bega, kisha ya tatu juu yao. Hizi kwa kawaida huwa nyekundu, ingawa kuna rangi nyingine (k.m. bluu). Rangi ya waridi, hata yenye maua, haidharauliwi na wapiganaji. Mavazi yanayojulikana kama kanga hupatikana kwa urahisi. Wamasai wanaoishi karibu na pwani huvaa kikoi, aina ya kitambaa inayopatikana katika rangi mbalimbali na nguo. Hata hivyo, mtindo uliopendelewa ni mistari.
|
20231101.sw_1701_68
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Wamasai wengi huko Tanzania huvaa makubadhi, ambayo walikuwa mpaka hivi majuzi wakizitengeneza kutoka ngozi ya ng'ombe kulinda nyayo. Siku hizi hutumia gurudumu au plastiki kuyatengeneza. Wanaume na wanawake huvaa vikuku vya mbao.
|
20231101.sw_1701_69
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Wamasai wanawake mara kwa mara hufuma marembesho na mikufu ya shanga. Ushanga huwa sehemu muhimu ya urembesho wa miili yao. Ingawa kuna tofauti katika maana ya rangi ya shanga, baadhi ya maana kwa jumla ya rangi chache ni: nyeupe, amani; bluu, maji; nyekundu, mpiganaji / damu / shujaa.
|
20231101.sw_1701_70
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Ushanga, unaofanywa na wanawake ina historia ndefu kati ya Wamasai, ambao hujitambulisha katika jamii kupitia mapambo ya mwili na uchoraji. Kabla ya kuwasiliana na Wazungu shanga zilikuwa zikitengenezwa kutoka vifaa vya kienyeji. Shanga nyeupe zilitengenezwa kutoka udongo, pembe, au mfupa. Shanga nyeusi na bluu zilitengenezwa kutoka chuma, makaa, mbegu, udongo, au pembe. Shanga nyekundu zilitengenezwa kutoka mbegu, mbao, maburu, mifupa, pembe, shaba, au chuma. Katika karne ya 19, shanga nyingi zenye rangi mbalimbali zilifika Afrika Mashariki kutoka Ulaya, zikabadilishwa na shanga za jadi na kutumiwa kutengeneza mipangilio bora ya rangi. Hivi sasa, shanga za kioo, bila urembesho hupendelewa.
|
20231101.sw_1701_71
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Kunyoa kichwa ni kawaida katika sherehe za kubalehe, kuwakilisha mwanzo mpya kutoka sura moja ya maisha hadi nyingine. Wapiganaji tu wanaruhusiwa kuwa na nywele ndefu, ambazo huzifuma katika nyuzi ndogondogo.
|
20231101.sw_1701_72
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Anapofikisha umri wa miezi 3, mtoto hupewa jina na kichwa hunyolewa safi, isipokuwa kifurushi cha nywele, kinachofanana na kilemba cha jogoo kutoka shingo hadi paji la uso. Ufananishi huu na jogoo humaanisha "hali ya neema" wanayopewa watoto wachanga. Mwanamke aliyepoteza mtoto awali alipokuwa akijifungua ataweka kifurushi hiki cha nywele mbele au nyuma ya kichwa, kutegemea kama alipoteza mvulana au msichana.
|
20231101.sw_1701_73
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Siku mbili kabla ya wavulana kutahiriwa, vichwa vyao hunyolewa. Kisha vijana mashujaa huruhusu nywele zao kukua, na hutumia muda mwingi wakisuka nywele. Nywele hizo hupakwa mafuta ya wanyama na mchanga mwekundu, na huhasimiwa juu ya kichwa kwa kipimo cha masikio. Nywele kisha husukwa: inagawanyishwa katika sehemu ndogo na kusongwa kwanza ikiwa imetenganishwa, halafu ikiwa imeunganishwa. Pamba au nyuzi za sufu zinaweza kutumiwa kurefusha nywele. Nywele zilizosukwa huweza zikaachwa zimelegea au zikafungwa pamoja kwa ngozi. Wakati wapiganaji kwenda kupitia Eunoto, na kuwa wazee, nywele zao ndefu zilizosukwa hunyolewa.
|
20231101.sw_1701_74
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Vilevile wanaume hunyoa nywele wanapopita kifungu kimoja cha maisha hadi kingine. Bibiarusi pia atanyolewa kichwa chake, na kondoo wawili dume watachinjwa kuzingatia sherehe hiyo.
|
20231101.sw_1701_75
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Sera za serikali, kama vile hifadhi na utunzaji wa akiba, na kutengwa kwa Wamasai, pamoja na kuongeza idadi, n.k. zimefanya vigumu kudumisha maisha ya Wamasai.
|
20231101.sw_1701_76
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Katika kuongezeka kwa umaskini na uhamiaji, mamlaka ya wazee wa jadi wa Kimasai inaonekana kudidimia.
|
20231101.sw_1701_77
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Kwa muda, miradi mingi imeanza kusaidia viongozi wa Kimasai kutafuta njia za kuhifadhi mila zao na pia kusawazisha mahitaji ya elimu ya watoto wao kwa dunia ya kisasa.
|
20231101.sw_1701_78
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Njia za ajira zinazojitokeza miongoni mwa Wamasai ni kilimo, biashara (kuuza dawa za jadi, biashara ya mikahawa / maduka, kununua na kuuza madini, kuuza bidhaa za maziwa na wanawake, nyuzi), na mshahara wa ajira (kama walinzi wa usalama / wapishi, kuongoza watalii), na wengine ambao wanahusika katika sekta mbalimbali.
|
20231101.sw_1701_79
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Wamasai
|
Wamasai
|
Wamasai wengi wameacha maisha ya wahamaji na kupata nafasi za kuwajibika katika biashara na serikali. Hata hivyo, licha ya maisha ya kisasa wanayoishi mjini, wengi hurudi nyumbani na nguo za kisasa, na hutoka kwenye familia yao wakiwa wamevalia shuka la kitamaduni (kitambaa cha rangi nyingi), patipati za ngozi ya ng'ombe, na fimbo ya mbao ('o-rinka') - wakihisi huru kwa wenyewe na dunia.
|
20231101.sw_1705_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ulaya
|
Ulaya
|
Ulaya (asili ya jina ni neno la Kiarabu ولاية, wilaayatun; inaitwa pia Uropa) ni bara lenye eneo la km² 10,600,000 tu, lakini wakazi ni milioni 747 .
|
20231101.sw_1705_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ulaya
|
Ulaya
|
Wengi wenye asili ya Ulaya wakati wa ukoloni walitawanyika duniani, hasa Amerika, wakiathiri kote upande wa lugha, utamaduni na dini.
|
20231101.sw_1705_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ulaya
|
Ulaya
|
Katika karne ya 20, baada ya vita kuu mbili, nchi mbalimbali za Ulaya zilianza kushirikiana kwa njia mbalimbali:
|
20231101.sw_1705_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ulaya
|
Ulaya
|
Katika orodha inayofuata kanda zinatajwa katika utaratibu wa Umoja wa Mataifa (UN categorisations/map). Lakini utaratibu huo haukubaliki ndani ya Ulaya kwa nchi za Ulaya ya Kati. Wajerumani, Waaustria, Waswisi, Wacheki, Waslovakia na Wapoland hukubaliana ya kwamba wenyewe si Ulaya ya Magharibi wala ya Mashariki ila Ulaya ya Kati. Kuna majadiliano kuhusu mipaka ya kanda hili yasiyokwisha bado, kwa mfano suala la Hungaria au Latvia.
|
20231101.sw_1705_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ulaya
|
Ulaya
|
1. Kanda zinazotajwa (Ulaya ya Kusini – magharibi n.k.) zinafuata utaratibu wa Umoja wa Mataifa UN categorisations/map. Nchi kadhaa zinazotajwa hapo chini zinaweza kuhesabiwa kuwa sehemu ya Ulaya na pia bara nyingine (Asia, Afrika, au Oceania). Hii inategemea na namna ya kugawa kontinenti; pia wakazi wenyewe wanaweza kujielewa tofauti na majirani yao.
|
20231101.sw_1705_5
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ulaya
|
Ulaya
|
2. Urusi ni nchi ya kontinenti mbili za Ulaya ya Mashariki na Asia; namba za wakazi na za eneo zimetasjwa kwa ajili ya sehemu ya Kiulaya pekee.
|
20231101.sw_1705_6
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ulaya
|
Ulaya
|
3–5. Guernsey, Kisiwa cha Man, and Jersey ni maeneo ya kujitegemea chini ya Taji la Ufalme wa Uingereza.
|
20231101.sw_1705_7
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ulaya
|
Ulaya
|
6. Namba za Ureno hazijumlishi Visiwa vya Madeira, ambazo ni sehemu ya Ureno magharibi ya Marokko katika Afrika.
|
20231101.sw_1705_8
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ulaya
|
Ulaya
|
7. Namba za Hispania hazijumlishi Visiwa vya Kanari magharibi ya Marokko katika Afrika, wa maeneo ya Ceuta na Melilla ambayo ni sehemu za Hispania kwenye pwani ya Moroko, Afrika ya Kaskazini.
|
20231101.sw_1705_9
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ulaya
|
Ulaya
|
8. Namba za Ufaransa hazijumlishi maeneo yake yaliyopo Amerika ya Kati au Kusini, Bahari Hindi au Oceania.
|
20231101.sw_1705_10
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ulaya
|
Ulaya
|
9. Uholanzi: Idadi ya wakazi ni ya 2004; Amsterdam ni Mji Mkuu lakini Den Haag ni makao makuuy a serikali.
|
20231101.sw_1705_11
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ulaya
|
Ulaya
|
10. Armenia huhesabiwa mara nyingi kuwa nchi ya kimabara katika Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) na Ulaya ya Mashariki
|
20231101.sw_1705_12
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ulaya
|
Ulaya
|
11. Azerbaijan huhesabiwa mara nyingi kuwa nchi ya kimabara katika Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) na Ulaya ya Mashariki; idadi ya wakazi na eneo zimetajwa za sehemu ya Ulaya pekee.
|
20231101.sw_1705_13
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ulaya
|
Ulaya
|
12. Kupro huhesabiwa mara nyingi kuwa nchi ya kimabara katika Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) na Ulaya ya Kusini; idadi ya wakazi na eneo zimetajwa za sehemu zisozo chini ya Dola ya Kituruki ya Cyprus.
|
20231101.sw_1705_14
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ulaya
|
Ulaya
|
13. Georgia huhesabiwa mara nyingi kuwa nchi ya kimabara katika Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) na Ulaya ya Mashariki; idadi ya wakazi na eneo zimetajwa za sehemu ya Ulaya pekee.
|
20231101.sw_1705_15
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ulaya
|
Ulaya
|
14. Uturuki ni nchi ya kimabara katika Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) na Ulaya ya Kusini; namba zinazotajwa zinahusiana na sehemu ndogo ya Magharibi pakee iliyomo Ulaya hasa jimbo lote la Istanbul.
|
20231101.sw_1705_16
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ulaya
|
Ulaya
|
15. Kazakhstan huhesabiwa mara nyingi kuwa nchi ya kimabara katika Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) na Ulaya ya Mashariki; idadi ya wakazi na eneo zimetajwa za sehemu ya Ulaya pekee.
|
20231101.sw_1706_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lituanya
|
Lituanya
|
Lituanya (au Lituania) ni nchi huru iliyoko Kaskazini Mashariki mwa Ulaya. Inajulikana rasmi kama Jamhuri ya Lituania.
|
20231101.sw_1706_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lituanya
|
Lituanya
|
Lituania kuanzia karne ya 13 ilikuwa nchi huru na imara iliyoteka maeneo mengi; kufikia karne ya 15, ikiwa pamoja na Polandi, ilikuwa kubwa kuliko nchi zote za Ulaya.
|
20231101.sw_1706_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lituanya
|
Lituanya
|
Wananchi kwa asilimia 84 wanaongea Kilituania ambacho pamoja na Kilatvia ndizo lugha hai pekee za jamii ya lugha za Kibaltiki kati ya lugha za Kihindi-Kiulaya. Ndiyo lugha rasmi.
|
20231101.sw_1706_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Lituanya
|
Lituanya
|
Dini ya wananchi ni Ukristo wa Kanisa Katoliki (77.2%), mbali ya Waorthodoksi (4.9%) na Waprotestanti (0.8%). Wasio na dini yoyote ni 6.1%.
|
20231101.sw_1707_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Europa
|
Europa
|
Europa (mitholojia), binti wa mfalme katika masimulizi ya dini ya Wagiriki wa Kale aliyekuwa mpenzi wa mungu mkuu Zeus
|
20231101.sw_1707_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Europa
|
Europa
|
Europa (kombora) ilikuwa kombora la Kiulaya la kurusha vyombo angani kabla ya kupatikaka kwa makombora ya Ariane
|
20231101.sw_1750_0
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shilingi
|
Shilingi
|
Asili ya jina ni kitengo cha kihistoria cha pesa katika nchi mbalimbali za Ulaya kama vile Austria, Uswisi, Uingereza, Poland, Denmaki, Norwei na Uswidi.
|
20231101.sw_1750_1
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shilingi
|
Shilingi
|
Katika nchi nyingi kati ya hizo pesa hiyo haikutumika tena isipokuwa hadi mwaka 1971 Pauni ya Uingereza ilikuwa na shillings 12 na kila shilling ilikuwa na penny 20. Nchi nyingi zilizorithi mfumo wa pesa kutoka Uingereza walitumia pauni na shilingi hadi kuhamia kwenye pesa ya desimali.
|
20231101.sw_1750_2
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shilingi
|
Shilingi
|
Uingereza ilitoa "East African Shilling" kuanzia mwaka 1921 kama pesa ya pamoja kwa ajili ya makoloni yake ya Kenya, Uganda na Tanganyika. Zanzibar ilijiunga na shilingi hiyo mwaka 1935 ilipoacha rupia zake.
|
20231101.sw_1750_3
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shilingi
|
Shilingi
|
Baada ya uhuru nchi hizo zilivunja umoja wa kifedha zikaanzisha pesa zao za pekee. Zote zinaitwa shilingi lakini thamani ilianza kutofautiana haraka, ya Kenya ikiongoza na ya Uganda kushika nafasi ya mwisho.
|
20231101.sw_1750_4
|
https://sw.wikipedia.org/wiki/Shilingi
|
Shilingi
|
Kuna majadiliano ya kurudisha shilingi ya pamoja kwa nchi za Jumuia ya Afrika ya Mashariki. Kwanza ilitarajiwa kuanzishwa mwaka 2012, halafu mwaka 2015, sasa mwaka 2024.
|
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.